Cambodia imetoa wito wa kusitishwa "mara moja" kwa mapigano na Thailand, kwani nchi hizo mbili zimeshuhudia zaidi ya watu 32 wakiuawa, wakiwemo raia, katika mapigano yanayoendelea mpakani.
Balozi wa Cambodia katika Umoja wa Mataifa, Chhea Keo, alisema nchi yake iliomba mapatano "bila masharti", akiongeza kuwa Phnom Penh pia alitaka "suluhisho la amani la mzozo huo".
Thailand haijatoa maoni hadharani kuhusu pendekezo hilo, huku ikikataa upatanishi wa watu wengine. Hapo awali ilitangaza sheria ya kijeshi katika wilaya nane zinazopakana na Kambodia.
Mapigano kwenye mpaka wa Thailand na Kambodia yamendelea hadi siku ya tatu na mambo mapya yaliibuka siku ya Jumamosi huku pande zote mbili zikitafuta uungwaji mkono wa kidiplomasia, kila upande ukisema umejilinda na kuutaka upande mwingine usitishe mapigano na kuanza mazungumzo.
Takriban watu 32 wameuawa na zaidi ya watu 130,000 wamekimbia makazi yao katika mapigano mabaya zaidi kati ya majirani wa Kusini Mashariki mwa Asia katika kipindi cha miaka 13.
Watu wakwa wamepumzika ndani ya makazi ya muda katika jimbo la Srisaket, baada ya Thailand na Cambodia kufyatuliana risasi kali kwa siku ya pili siku ya Ijumaa huku mapigano ya mpakani yakizidi na kuenea, huku kiongozi wa Kambodia akisema Thailand imekubali pendekezo la Malaysia la kusitisha mapigano lakini ikarudi nyuma,
Jeshi la majini la Thailand lilisema kulikuwa na mapigano katika jimbo la pwani la Trat mapema Jumamosi, eneo jipya zaidi ya kilomita 100 (maili 60) kutoka maeneo mengine ya vita kwenye mpaka unaopiganiwa kwa muda mrefu.
0 Comments