Header Ads Widget

KALENDA YA UCHAGUZI MKUU 2025 YAZINDULIWA RASMI

 

Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima Media Dodoma

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza rasmi Kalenda ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 29 kwa ajili ya kuwachagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na Madiwani kwa upande wa Tanzania Bara.

Akizungumza jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Jakobo Mwambegele amesema Kalenda hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Kanuni mbalimbali ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa uwazi, haki na kwa mujibu wa sheria.

Amesema Tarehe 9 Agosti hadi 27 Agosti 2025 ni kipindi cha utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Aidha ameeleza kuwa tarehe 14 Agosti hadi 27 Agosti 2025 ni kipindi cha utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani


Pia  amesema tarehe 27 Agosti 2025 ni siku rasmi ya uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais pamoja na uteuzi wa wagombea wa Ubunge na Udiwani



Ameeleza tarehe 28 Agosti hadi 28 Oktoba 2025 ni kipindi rasmi cha kampeni za Uchaguzi kwa upande wa Tanzania Bara


Amesema ,Tarehe 28 Agosti hadi 27 Oktoba 2025 ni kipindi cha kampeni kwa upande wa Zanzibar ili kupisha maandalizi ya kura ya mapema


Amesema ,Tarehe 29 Oktoba 2025 ambayo ni siku ya Jumatano ni siku rasmi ya upigaji kura kwa wananchi wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


 "Nitoa wito kwa vyama vya siasa wagombea mashirika ya kiraia waangalizi wa uchaguzi vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia sheria maadili na taratibu zilizowekwa, "Amesema Jaji Mwambegele


 Na Kuongeza " Amesisitiza kuwa Tume itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani huru na wa haki huku haki ya kila mpiga kura na mgombea ikilindwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi, "


Amesisitiza kuwa Tume itatoa elimu kwa umma kuhusu haki ya kupiga kura wajibu wa wananchi na umuhimu wa kudumisha amani kabla wakati na baada ya uchaguzi


Hata hivyo Mwenyekiti huyo aliwasilisha Majina ya watu 8703 kwa Jeshi la Polisi nchini kutokana na kujiandikisha zaidi ya mara moja Katika Daftari la kudumu la wapiga kura ambapo ni kinyume cha Sheria. 



"Kufanya hivyo nikinyume na sheria ya uchaguzi hivyo majina hayo yanafikishwa sehemu inayohusika, " Amesema


Nao baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa wametoa maoni yao kuhusiana na uchaguzi Mkuu.


Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Doyo Hassan Doyo, Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD) na mgombea urais kupitia chama hicho, amesema kuwa hatua ya Tume kuwaita wadau mbalimbali na kuwashirikisha katika tukio hilo ni tofauti kabisa na miaka ya nyuma ambapo taarifa za uchaguzi zilitolewa kupitia vyombo vya habari pekee bila majadiliano ya pamoja.


“Leo ni tukio kubwa na la kihistoria. Tunampongeza sana Mkurugenzi pamoja na Mwenyekiti wa Tume kwa hatua ya kutushirikisha tangu mwanzo. Kutoka moyoni tunakwenda kushiriki uchaguzi tukiwa na imani kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi itasimamia haki na kutekeleza kwa vitendo dhamira waliyoionesha,". 


Na kuongeza "Tumekuwa sehemu ya kila hatua kuanzia uboresha wa daftari la wapiga kura, kusaini maadili ya uchaguzi hadi leo hii ambapo tarehe ya uchaguzi imepangwa kwa uwazi,” amesema Doyo.


Naye Dkt Eveline Munisi, Katibu Mkuu wa chama cha NCCR Mageuzi, amesema kuwa baada ya Tume kupuliza kipenga rasmi cha Uchaguzi Mkuu, chama chake kiko tayari na tayari kilianza maandalizi mapema kuhakikisha kinashiriki kikamilifu.


“Sisi NCCR Mageuzi tumekuwa tayari hata kabla ya tangazo rasmi la tarehe ya uchaguzi. Tayari tumeshampata mgombea urais na mgombea mwenza, na hadi kufikia muda huu tumeshapokea watia nia wa majimbo karibu 2,000 kwa ngazi ya kata, idadi ya watia nia ni kubwa mno,” amesema Dkt Munisi.


Hata hivyo jumla ya Vituo zaidi ya elfu97 vitatumika kupigia kura Tanzania Bara huku Zanzibar vitatumika jumla ya vituo 500.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI