Na Pamela Mollel, Arusha
Wanahabari wa Afrika wametakiwa kuandika habari chanya zenye kuleta tija kwa bara la Afrika badala ya kutegemea taarifa kutoka vyombo vya nje.
Wito huo umetolewa Juni 15, 2025 jijini Arusha na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa mabaraza huru ya habari barani Afrika.
Dkt. Mpango alisisitiza kuwa ni muhimu kwa mabaraza ya habari kuandaa mapendekezo ya kisera na kisheria yatakayosaidia kusimamia matumizi bora ya akili bandia (AI) kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Kwa upande wake, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, alipokea tuzo maalum kwa niaba ya Hayati Ali Hassan Mwinyi kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuanzisha vyombo binafsi vya habari nchini.
Dkt. Mwinyi alieleza kuwa vyombo vya habari ni muhimu sana katika kuwezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.
Katika baraza hilo pia, Madaraka Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa, alipokea tuzo ya miaka 30 kwa niaba ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere, kwa mchango wake katika kukuza uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata taarifa.
0 Comments