Na Mwandisho wetu, Bariadi.
MAKATIBU Tawala Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Geita inayounda kanda ya ziwa mashariki, Wametembelea, Kukagua na kuridhishwa na maandalizi katika eneo la maonyesho ya Nanenane Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Akiongoza ukaguzi huo, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Prisca Kayombo pamoja na viongozi wengine wakiwemo Makatibu Tawala Wasaidizi wa sehemu ya uchumi na uzalishaji, waratibu wa nanenane wa mikoa, wawakilishi wa makampuni binafsi pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Umma Mkoani Simiyu.
Maadhimisho ya sherehe za Nanenane yataanza rasmi Tarehe 1 Agosti 2025 na kuhitimishwa na kilele chake Tarehe 8 Agosti 2025 katika Viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi.
Mwisho.
0 Comments