NA MATUKIO DAIMA MEDIA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, William Lukuvi ametoa rai kwa wa-tumishi wa Wizara ya Nishati ku-hakikisha wanatunza miundombinu na vifaa vilivyopo katika jengo lao, ili vidumu kama ilivyokusudiwa.
Alitoa agizo hilo jana mkoani Dodoma baada ya kufanya ziara katika mji wa serikali ya Mtumba, iliyolenga kukagua jengo jipya la wizara hiyo ambalo limekamilika.
Lukuvi alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba, Naibu Katibu Mkuu, Dk. James Mataragio pamoja na mene-jimenti ya wizara.
Akiwa eneo hilo, Lukuvi aliipongeza menejimenti ya Wizara ya Nishati kwa uamuzi wa kuhamia rasmi katika mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma.
"Nakupongeza sana Ka-tibu Mkuu kwa hatua hii, pamoja na mkandarasi wa jengo na msimamizi, pia pia nawapongeza kwa nia thabiti ya kuhamia
katika mji huu wa serikali baada ya Rais Samia Suluhu kutoa fedha zilizowezesha ujenzi wa majengo haya," alisema Lukuvi
Alisema nia ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa ufanisi ka-tika eneo moja na hivyo kuondoa usumbufu wa kutumia muda mrefu kupata huduma katika maeneo tofauti.
Lukuvi alisema: "Nawashukuru sana wizara kwa kumheshimisha Rais Samia Suluhu Hassan, kwa sababu nia yake ni watumishi kuwa pamoja katika utoaji wa hu-duma ili kuleta ufanisi." Kadhalika, alimpongeza Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko kwa kuweka msukumo kwa wizara katika kukamilisha jengo hilo na kwa watumishi kuhamia katika jengo husika.
Hivi sasa idara na vitengo vyote vya Wizara ya Nishati vimeshahamia katika jengo la wizara hiyo lililopo katika mji huo wa serikali.
0 Comments