Header Ads Widget

KESI YA LISSU YAHAIRISHWA HADI AGOST 13,2025.

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

DAR ES SALAAM.Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga, ameahirisha kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, hadi tarehe 13 Agosti 2025, huku akitoa angalizo kwa upande wa Jamhuri kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha Mahakama Kuu inatoa uamuzi kuhusu maombi ya kulinda mashahidi.

Akiwa mbele ya Mahakama hiyo, Hakimu Kiswaga amesema amekuwa na utaratibu wa kutoa maamuzi moja kwa moja, lakini safari hii amehitaji muda zaidi kufanya utafiti wa kisheria kutokana na uzito wa hoja za pande zote.

"Sasa ninaahirisha kesi hii ili nijipe muda zaidi wa kufanua utafiti wa kisheria na kuja na maamuzi madogo, kwahiyo leo sitatoa maamuzi madogo. Ninaahirisha mpaka tarehe ijayo, hoja zilizotolewa na pande zote mbili zinahitaji muda wa kutosha, kwasababu pia authorities ambazo zimekuwa cited zimekuwa ni nyingi na zenye kujirudiarudia, mahakama inahitaji muda", amesema Hakimu Kiswaga.

Upande wa Jamhuri uliiomba Mahakama hiyo kusubiri uamuzi wa Mahakama Kuu kabla ya kuwasilisha hati ya mashtaka au taarifa ya mashtaka dhidi ya Lissu. Wakili wa Serikali Mkuu, Nassor Katuga, alieleza kuwa maombi hayo ya ulinzi kwa mashahidi yaliwasilishwa Mahakama Kuu na kupewa tarehe ya kusikilizwa Agosti 4, 2025.

Kwa mujibu wa Katuga, maelezo ya mashahidi yanapaswa kuambatana na taarifa ya mashtaka, jambo lililochelewesha mchakato huo kutokana na mashahidi hao kuwa sehemu ya ombi la ulinzi.

Awali, Tundu Lissu alieleza masikitiko yake juu ya mfululizo wa kuahirishwa kwa kesi hiyo, akidai kuwa mawakili wa serikali wanatumia mwanya huo kuendelea kumuweka mahabusu kwasababu isiyo na msingi.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI