Header Ads Widget

CCM WABARIKI MAREKEBISHO YA KATIBA

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Chama cha Mapinduzi kimeamua kufanya marekebisho ya Katiba kwenye upande wa majina ya Watu walioomba kugombea Ubunge na Udiwani ambapo licha ya majina ya Wagombea wanaoteuliwa ngazi ya Kamati za Siasa za Wilaya na Mkoa kubaki matatu kwa kila Jimbo na Kata, kwa marekebisho ya Katiba, Kamati Kuu itakuwa na uwezo wa kubadilisha maamuzi endapo itaamua vinginevyo.


Akisoma marekebisho hayo kwenye mkutano mkuu leo July 26,2025 Jijini Dodoma, Katibu wa NEC- Organizesheni Issa Haji (Gavu), amesema “Imependekezwa marekebisho ya ibara ya 105 ibara kuu ya 7 F kwa kuongeza maneno ‘isipokuwa kama Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itaamua vinginevyo’ hivyo Ibara ya 105 ibara kuu ya 7 F ya CCM inapendekezwa isomeke kama ifuatavyo ‘Kufikiria na kuteua majina ya Wana CCM wasiozidi watatu kwa kila Jimbo la uchaguzi walioomba nafasi ya Ubunge na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi ili wakapigiwe kura isipokuwa kama Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itaamua vinginevyo’

“Kwa upande wa udiwani inapendekezwa kufanya marekebisho kwenye ibara ya 91 6C  kwa kuongeza maneno isipokuwa kama Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itaamua vinginevyo hivyo mapendekezo yatasomeka ‘kwa upande wa udiwani itafikiria na kuteua majina ya Wana CCM wasiozidi watatu kwa kila Kata ili wakapigiwe kura za maoni isipokuwa kama Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itaamua vinginevyo”

Itakumbukwa kuwa kwa marekebisho ambayo yalifanywa katika mkutano mkuu uliopita, Kamati Kuu kwa sasa isingekuwa na mamlaka ya kuteua jina la Mgombea yoyote nje ya wale watatu waliopendekezwa na Kamati za siasa za Wilaya na Mikoa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI