Na WILLIUM PAUL, VUNJO.
WATER wa mila wa kabila la Wakahe na Wamaasai kutoka Kata ya Kahe Magharibi, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngasini, Goodluck Meshack Mlay, pamoja na Andasoni Kireja, Godsoni Samweli, Peter Melisoki na Laigwanani David Laiza, wamemkabidhi heshima maalum Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei.
Katika tukio hilo lenye utamaduni na heshima ya pekee, wazee hao walimvisha Dkt Kimei shuka la Kimaasai, ishara ya heshima, kumbariki na kumzawadia mbuzi dume kama shukrani kwa kazi kubwa ya maendeleo aliyotekeleza katika kata hiyo.
Hafla hiyo ilifanyika sambamba na mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020–2025, ambapo viongozi na wajumbe wa mkutano huo kwa kauli moja walimtaka Dkt Kimei kuchukua fomu ya kuwania tena Ubunge wa Jimbo la Vunjo mwaka huu, wakisisitiza kuwa maendeleo yaliyofanyika yanahitaji kuendelezwa kwa kasi zaidi chini ya uwakilishi na uongozi wake.
Tukio hilo limethibitisha kuungwa mkono kwa Dkt Kimei kutoka ndani ya CCM, jamii za asili, wazee wa mila, na wananchi wa kawaida, kama kielelezo cha mshikamano, utulivu na matumaini ya maendeleo endelevu kwa Vunjo.
MWISHO..
0 Comments