Na WILLIUM PAUL, VUNJO.
MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei amekabidhi mchango wa shilingi milioni tano (5,000,000) kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Kahe Magharibi, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake kwa wanachama na viongozi wa kata hiyo.
Mchango huo umetumwa kwenye akaunti ya CRDB ya Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo, Zablon Nguma.
Dkt Kimei alitoa ahadi hiyo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020–2025, na leo ameitimiza rasmi wakati wa mkutano wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha miaka mitano.
Mchango huo umetafsiriwa kama ishara ya uaminifu na uongozi wa mfano, huku ukiakisi dhamira ya kweli ya Dkt Kimei ya kuijenga CCM kuanzia ngazi za msingi, na kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi wa Chama katika Kata hiyo.
MWISHO..
0 Comments