Header Ads Widget

TANESCO YAZINDUA KAMPENI YA ULIPAJI MADENI NA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME

 

Na Fatma Ally Matukio DaimaApp 


Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) leo limezindua kampeni maalum kwenye maeneo yote nchini ya kuhamasisha ulipaji wa madeni kutoka kwa wateja wa malipo baada ya ukaguzu wa mita za LUKU kwa wateja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa TaNESCO ,Irene Gowelle amesema kampeni hiyo imelenga kuwahamasisha wateja wa malipo ya baada kulipa madeni yao kwa hiyari kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa na kutoa madeni yao kikamilifu.

Aidha, amesema zoezi hio pia litaenda sambamba na kuhamasisha ulinzi wa miundombinu ya umeme ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha na kuimarisha uendelevu wa upatikanaji huduma bora ya umeme kwa wananchi.

"Zoezi hili pia litahusisha ukaguzi wa mita za Luku kwa lengo la kuhakikisha zinafanya kazi vizuri na hazijachezewa na wateja wasio waaminifu, kauli mbiu yake " Huduma endelevu huanza na wewe",amesema

Aidha, pia imelenga kuhamasisha umuhimu wa ulinzi shirikishi wa miundombinu ya umeme kwa kuwajumuisha wananchi na kuwapa elimu ya kulinda miundombinu ya Shirika, miundombinu hii ndio inayowewezesha upatikanaji endelevu wa huduma ya umeme kwa ufanisi hasa kwa kuzingatia kuwa ulinzi wa Miundombinu ya umma ni wajibu kila mwananchi.

Sanjari na hayo pia ameeleza  kwamba Tanesco  inatoa rai kwa  wateja wake wote nchini ambao  wanadaiwa kutoa ushirikiano kwa kulipa madeni yao kwa wakati na hivyo kutoathiri upatikanaji wa  huduma ya umeme kwenye shughulu zao.

Sambamba na hayo Tanesco pia inatoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kuhusu vitendo vya wizi wa umeme au uharibifu na wizi wa  miundombinu ya umeme kwa kushirikiana na vyombo vya dola Ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kwa ukosefu wa huduma ya umeme pamoja na kuzuia hasara kwa Shirika.

Aidha, kampeni hiyo imekwenda sambamba na kauli mbiu ya "Lipa deni,Linda Miundombinu,Tukuhudumie"ikienda sambamba na kauli mbiu isemayo "Huduma endelevu huanza na wewe"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI