Header Ads Widget

SERIKALI KUJENGA DARAJA KUTOKA MKOKOTONI HADI TUMBATU

Na Matukio Daima App.

Serikali  ya Mapinduzi  ya Zanzibar  imesema kuwa  ipo katika hatua za mwisho za kufanya upembuzi yakinifu ya ujenzi wa Daraja linalounganisha Mkokotoni hadi  kisiwa cha Tumbatu yenye urefu wa wastani wa kilomita 2.

Aidha Serikali ipo katika za kuanza ujenzi wa Barabara  itakayounganisha Mkoa wa Kaskazini  Unguja  na Mkoa wa kusini Unguja kutoka Nungwi hadi Paje.

Akizungumza  na Waandishi wa Habari leo Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usimamizi na utumzaji aa Barabara  Zanzibar  Injinia Cosmas  amesema Serikali imedhamiria kuunganisha maeneo mbalimbali   kwa ujenzi wa barabara  na madaraja katika  visiwa vidogo vidogo ili kurahisha huduma za usafirishaji nchini.

"Tunasubiri ripoti ya upembuzi yakinifu ili kuona kuna uwezekano wa ujenzi wa Daraja kutoka Mkokotoni hadi Tumbatu ambapo tunaamini ujenzi wa Daraja hili utakifungua zaidi kisiwa cha Timbatu kiuchumi," amesema.

"Kwa sasa tayari tumeshaanza ujenzi wa Barabara  zaidi ya kilomita 15 ndani ya kisiwa cha Tumbatu jambo  ambalo hakuna alietarajia," 

Ameeleza kuwa, Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2025-2030 inawaelekeza kujenga Barabara itakayowaunganisha Wananchi kutoka Kaskazini Unguja hadi Kusini ili kuondia adha ya usafiri pamoja na ujenzi wa barabara za mjini na za ndani katika maeneo ya Unguja na Pemba .

"Muda wowote kuanzia sasa tunaanza ujenzi w Barabara Barabara  kutoka Nungwi Kaskazini  Unguja  hadi Paje Kusini Unguja," ameeleza.

"Kisiwani Pemba hatukuwa nyuma katika utekelezaji wa Ilani maana tuneshakamilisha ujenzi wa Barabara  kuu na Barabara za ndani na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ya kikufungua kisiwa cha Pemba,"  Amesema.

Amesema ujenzi wa Barabara  ya Wete chake unaendelea kwa kasi huku Ujenzi wa Barabara  ya Mkoani Chake - chake ukitarajiwa kuanza hivi karibuni kama Ilani ya Uchaguzi  inavyoelekeza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI