Mhandisi Mathias Mwenda Meneja wa RUWASA mkoa Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Wakala wa maji vijijini na usafi wa mazingira (RUWASA) mkoa Kigoma umeeleza kuvutia na teknolojia ya ukusanyaji wa takwimu za uzalishaji maji unaotumia mfumo wa Computer kupitia satellite ambapo watendaji wa wakala huo wanaweza kupata takwimu za uzalishaji maji kwenye maeneo yake mbalimbali wakiwa ofisini.
Meneja wa RUWASA mkoa Kigoma,Mhandisi Mathias Mwenda alisema hayo wakati mameneja na watendaji waandamizi wa RUWASA kutoka wilaya zote za mkoa Kigoma walipofanya ziara kutembelea mradi wa maji katika kijiji cha Makere wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma uliotekelezwa na Shirika la Water Mission kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF).
Ziara hiyo imekuja baada ya kikao cha siku nne cha viongozi hao chini ya Water Mission na UNICEF kwa ajili ya kufanya tathmini ya usanifu, utekelezaji na uendeshaji wa huduma za maji baada ya kukamilika kwa miradi ambapo walitembelea mradi huo unaotumia mfumo wa satellite kupata takwimu za kila siku za uzalishaji maji katika mradi huo.
Mhandisi Mathias Mwenda alisema kuwa iwapo RUWASA itaweka mfumo huo katika miradi ya maji inayotekeleza na kukamilika itawapa nafasi nzuri ya kujua kama mradi unafanya kazi au umesimama kutokana na takwimu kuonyesha kwama uzalishaji upo au haupo hivyo wanafikiria kuishauri serikali kuona namana ya kuuchukua mfumo huo na kuutekeleza kwenye miradi yao.
Naye Meneja wa RUWASA wilaya ya Kibondo, Mohamed Almasi alisema kuwa mfumo huo ni mzuri kwani wanaweza kukusanya takwimu za uzalishaji maji kutoka maeneo mbalimbali wakiwa ofisini na hivyo hadi wanapotaka kwenda kwenye maeneo ambayo hayaonyeshi uzalishaji wanakuwa wameshapata taarifa mapema za changamoto zilizopo.
Awali akiwatembeza katika mradi huo Meneja miradi kutoka Shirika la Water Mission,Denis Aborgast alisema kuwa mradi huo wa ukusanyaji takwimu za uzalishaji maji ni sehemu ya kuonyesha namna uendeshaji wa huduma za maji vijijini unaofanywa na kamati za jamii za uendesha huduma za maji vijijini (SIBIUSO) zinaweza kusimamiwa kwa watendaji wa RUWASA kutokuwepo kwenye eneo la utoaji huduma lakini huduma zakawa endelevu na kuwafanya kujua kama mradi unachangamoto.
Mwisho.
0 Comments