Header Ads Widget

RC MTAMBI ATAMANI MABILIONEA WATOKE MARA KUPITIA SEKTA YA MADINI

 

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amesema kama ataendelea kuwepo mkoa wa Mara atahakikisha wanapatikana mabilionea kupitia sekta ya madini.

Kauli hiyo ameitoa leo juni 3,2025 kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo wakati wa ufunguzi wa maonyesho na kongamano kuhusu masuala ya madini.

Amesema mkoa wa Mara una hazina kubwa ya rasilimali nyingi lakini upande wa madini wataibuka mabilionea watakao uinua juu zaidi mkoa huo.

Kanali Mtambi amewaambia wachimbaji wadogo na wakubwa wanaofanya shughuli za uchimbaji kwenye mkoa huo kuwa watumie fursa ya madini yaliyopo mkoani Mara kujiinua kiuchumi.

Amesema ndani ya siku 4 za maonyesho na kongamano la madini kuzitumia kujifunza teknolojia bora ya uchimbaji na kuchimba kwa tija.

Mkuu huyo wa mkoa wa Mara amesema hakuna shaka ya kupatikana kwa mabilionea hao kwa kuwa madini yapo na yakichimbwa kwa tija mafanikio yataonekana.


Amesema vijana wasidanganywe na mtu yoyote wakiwemo wanasiasa kwani serikali ipo karibu nao na kuwasaidia masuala mbalimbali kwenye sekta ya madini.


" Mimi kama mlezi wa wachimbaji na nikiendelea kuwepo mkoani Mara ntahakikisha wanazalishwa mabilionea hapa watakaoweza kuupandisha juu zaidi mkoa kwa ujenzi na vitega uchumi vya kisasa.


" Tutumie maonyesho na kongamano litakalofanyika kesho pale Mwembeni Complex kujifunza teknoloj

Ia mpya za uchimbaji ili tuwe wachimbaji bora",amesema.


Amesema ndani ya siku hizo yatafanyika matembezi ya wachimbaji kumuunga mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyorudisha shughuli za madini kwa wachimbaji wenyewe.


Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Mara Amini Msuya amesema shughuli za madini mkoa wa Mara zinakwenda vizuri hasa kwenye makusanyo.


Amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025 walipangiwa kukusanya bilioni 176 na hadi kufika mwezi uliopita wamekusanya bilioni 172 sawa na asilimia 98.


Amesema wanao uhakika wa kuvuka lengo la ukusanyaji kwa kuwa bado kuna mwezi mmoja mbele wa mwaka wa fedha na kudai katika kipindi kijacho wameongezewa kiwango cha makusanyo kufikia bilioni 210.


Katibu wa Shirikusho la Wachimbaji Wadogo Tanzania( FEMATA) Rogers Michael ameishukuru serikali kwa kuwathamini wachimbaji na kuwasaidia masuala mbalimbali.


Amesema kwa upande wa serikali ya mkoa wa Mara imekuja na kasi kupitia mkuu wa mkoa Kanali Evans Mtambi na watafanya vizuri kupitia sekta ya madini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI