Header Ads Widget

NJEZA AZIDI KUIBANA SERIKALI BARABARA YA MCHEPUKO, ISYONJE KIKONDO.



Na Matukio Daima App.

Wizara ya uchukuzi imesema inaendelea kutafuta fedha ili kuanza ujenzi wa barabara ya mchepuko kutoka Uyole hadi Songwe viwandani wilayani Mbeya na kwamba wananchi waliopisha barabara hiyo watalipwa fidia.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Naibu Waziri wa uchukuzi Mhe. David Kihenzile wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza.

Hata hivyo katika swali lake Mhe. Oran Njeza aliiuza Wizara ya Ujenzi juu ya fidia za wananchi wanaopisha ujenzi wa Barabara ya mchepuko (Baypass) huku pia akitaka kujua ni lini Ujenzi wa barabara ya Isyonje hadi kikondo utaanza.


Akijibu hayo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe David Mwakiposa Kihenzile amesisitiza kuwa ujenzi wa barabara kutoka Isyonje kikondo hadi Makete mkoani Njombe unaendelea na ulianzia eneo la Makete Njombe ambako kuna kilomita nyingine kwenda mkoani Mbeya na kwa upande wa kuanzia Isyonje hadi Kikondo anasema usanifu wa kina umeanza na kwamba uhakika barabara hiyo itajengwa na ujenzi unaendelea.

Kuhusu fidia kwa wanaopisha barabara ya mchepuko kutoka Uyole anasema wananchi wanaopisha ujenzi huo wanaendelea kulipwa kwa kadri ya upatikanaji wa fedha na mpaka sasa shilingi billion kumi zimeshalipwa hivyo kuwaondoa mashaka wananchi ambao bado hawajalipwa.

Mradi huu unagusa wananchi wa kata mbalimbali kupisha barabara kubwa kwa ajili ya magari makubwa (malori) na itagusa kata mbalimbali hasa za Mbeya vijijini ikiwemo kata ya Ijombe, Bonde la Songwe, Iwindi, Inyala na Swaya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI