Header Ads Widget

MATUMIZI SHERIA YA MANUNUZI YASISITIZWA KWENYE MIRADI YA UJENZI

 

Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Hassa Rugwa akizungumza katika kikao cha wakuu wa Taasisi, wakuu wa vitengo vya ugavi na manunuzi kutoka mikoa mitano ya kanda ya Magharibi kilichofanyika mkoani Kigoma

Meneja wa  PPRA kanda ya Magharibi, Bibi Suma Mwanjwango

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WAKUU wa Taasisi na wakuu wa vitengo vya ugavi na manunuzi katika mikoa ya kanda ya Magharibi wametakiwa kutekeleza takwa la kisheria la kutumia asilimia 30 ya fedha zinazokwenda kwenye miradi ya ujenzi baadhi ya kazi  kufanywa na vikundi vya kijamii.


Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Hassan Rugwa alitoa maagizo hayo mjini Kigoma alipokuwa akifungua kikao cha siku mbili cha viongozi hao kutoka mikoa ya Singida, Shinyanga, Katavi,Tabora na Wenyeji Kigoma kikao kilichoandaliwa na Mamlaka ya udhiti wa ununuzi wa umma (PPRA)


Rugwa alisema kuwa pamoja na sheria na taratibu za miradi ya ujenzi kutoa maelekezo hayo lakini bado miradi mingi inafanyika bila vikundi vya kijamii kunufaika na fursa hiyo ambayo lengo lake kuongeza mzunguko wa fedha kwenye maeneo ambayo miradi infanyika.



Awali Meneja wa  PPRA kanda ya Magharibi, Bibi Suma Mwanjwango alisema kuwa kikao hicho kimekuja baada ya mkoa Kigoma kuonekana uko nyuma katika kutekeleza sheria ya manunuzi ya umma katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi sambamba na tenda za ununuzi serikalini ambapo bado vikundi vya kijamii havijafaidika na fursa hiyo.


Mwanjwango alisema kuwa mkutano huo wa siku mbili utatoka na maazimio ya hatua za kuchukua baada ya kufanya tathmini ya hali ilivyo sasa na changamoto inayojitokeza kushindwa kutekelezwa kwa utaratibu huo.


Akizungumza katika kikao hicho Meneja wa Wakala wa barabara mkoa Kigoma (TANROADS),Mhandisi Narcis Choma alisema kuwa fedha kwa ajili ya asilimia 30 ya kuvipa vikundi kushiriki kwenye miradi ya ujenzi zipo lakini vikundi vingi vinavyoomba havijafikia vigezo vilivyoainishwa.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI