Na Shomari Binda-Musoma
MAFANIKIO mazuri ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba katika ziwa Victoria kwa wavuvi wa Musoma Vijijinj yameanza kuonekana.
Hivi karibuni mvuvi mmoja wa Kijijini Kigera Kitongoji cha Kurukiri amevuna samaki takribani tani 40 kutoka kwenye vizimba vyake 4 vyenye upenyo wa mita 10.
Taarifa iliyotolewa jana juni mosi na ofisi ya .bunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo imesema hayo ni mafanikio na makubwa zaidi yanakuja
Taarifa hiyo imesema masoko ya samaki wanaovunwa kutoka kwenye vizimba yapo ambayo ni ya walaji na viwanda vya minofu ya samaki.
Bei ya mazao hayo ya samaki inaendana na ukubwa na uzito wa samaki na kwa sasa ni kati ya shilingi 7,000 na 10,000 kwa kilo moja.
Ili kuhakikisha wanapatika wavuvi wengi wa vizimba na kuwainua kiuchumi taarifa hiyo imeeleza mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amekuwa mfatiliaji wa mikopo nafuu kitoka benki ya CRDB na NMB kuwafikia wavuvi na kuanzisha uvuvi huo.
" Ndani ya Kata zetu 21 Kata 18 zimezungukwa na ziwa Victoria na tunaendelea kufanya uhamasishaji wa uvuvi wa vizimba kwa wananchi wetu.
" Mafanikio yameanza kuonekana kutokana na kuvuliwa kwa samaki wengi huko kwenye Kijiji cha Kigera na maeneo mengine",imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Wavuvi na wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kutoa shukrani nyingi kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha njia kwa vitendo, ya uwekezaji mkubwa kwenye uvuvi wa vizimba nchini
0 Comments