Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania ambaye pia ni Askofu wa Jimbo wa Makanisa International Evangelism Mchungaji Maasa Ole Gabriel amewataka viongozi wa dini kueafundisha waumini wao kuwa wazalendo na wenye kuipenda nchi yao.
Askofu maasa ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa Kanisa la International uliofanyika makao Makuu ya kanisa hilo Sakila Wilayani Arumeru ambapo amesema pamoja na jukumu kubwa walilonalo viongozi wa dini pia wanapaswa kueafundisha wananchi uzalendo hasa kuelekea katika uchaguzi mkuu Oktoba 2025.
Akifungua Mkutano huo Askofu Mkuu wa Makanisa ya International Evangelism Mch.Eliudi Isangya amesema pamoja na mkutano huo kufanyika kila mwaka kujadili mambo mbalimbali,kwa mwaka huu wameazimia kuionbea nchi kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba.
Awali akihubiri kwenye ufunguzi wa Mkutano huo Askofu Ayubu Murini kutoka Kanda ya ziwa Jimbo la shinyanga kanisa la International kahama amewataka viongozi hao wa dini na waumini wote kutambua Nguvu ya Roho.Mtakatifu na jinsi ya kuipokea ambapo amesema Roho Mtakatifu kama pumzi ya Mungu inalikusanya kanisa na kuliweka mahali pamoja.
Mkutano huo mkuu umejumuisha maaskofu,wachungaji na viongozi wengine wa Makanisa ya International Evangelism kutoka mikoa yote Tanzania na nchi jirani.
0 Comments