Na Shomari Binda-Musoma
Kada wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Jumanne Munema ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Musoma mjini mbele ya mbunge Vedastus Mathayo.
Nia hiyo ameitangaza leo juni 13 2025 kwenye kikao kilichofanyika kwenye Kata ya Mwisenge wakati mbunge huyo akiwashukuru wana CCM kwa kumpa ushirikiano kwa kipindi cha uongozi wake unaokŵenda kumalizika.
Akizungumza kwenye kikao hicho amesema yapo mambo mazuri yaliyofanywa na mbunge huyo ambayo yanastahiki kupongezwa.
Munema amesema chama hakizuii mwanachama kugombea muda wa uchaguzi ukifika lakini pale yanapofanywa mazuri na mtangulizi hakuna budi kupongeza.
Amesema ameamua kutia nia ya kugombea ubunge ili kuendelea kusaidiana kuleta maendeleo ndani ya jimbo la Musoma mjini.
" Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mbunge wetu Vedastus Mathayo yapo mazuri ambayo ameyafanya.
" Musoma ile ya zamani sio Musoma hii ya leo yapo Mambo yamefanyika na kila mwana CCM anapaswa kutembea kifua mbele",amesema.
Munema amesema juni 28,2025 atachukua fomu ndani ya chama kugombea na kama itawapendeza na kumpongeza Mungu anaomba wamchague.
Akizungumza kwenye kikao hicho mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema hazuiliwi mwanachama kuhombea bali asibeze maendeleo yaliyofanyika.
0 Comments