Header Ads Widget

ILANI MPYA YA CCM 2025–2030 INAHESHIMISHA CHAMA, RAIS SAMIA NJIA NYEUPE – JASMIN NG'UMBI

 

Na Matukio Daima Media

 MJUMBE wa kamati ya utekelezaji umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Jasmin Ng'umbi , ameelezea matumaini na imani kubwa juu ya ilani mpya ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030.

 Akizungumza na Matukio Daima, Jasmin  alisema kuwa ilani hiyo imejaa mambo makubwa na mazuri ambayo yatakiimarisha chama hicho mbele ya wapiga kura na kuongeza heshima ya CCM mbele ya macho ya Watanzania.

 Alieleza kuwa, kama ilivyokuwa ilani ya uchaguzi ya awali, utekelezaji wa ilani hii mpya unaashiria mwendelezo wa mafanikio yaliyokwisha kupatikana, hasa katika sekta ya miundombinu, ajira, uchumi na utawala bora.


Jasmin  alisema kuwa wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla, hasa wakazi wa wilaya ya Kilolo, wana imani kubwa na ilani hiyo kutokana na namna ilani ya awali ilivyotekelezwa kwa mafanikio. 


Alitolea mfano ujenzi wa barabara za lami miradi ya afya na mingine ambayo  ni mojawapo ya mafanikio ya ilani ya mwaka 2020–2025.

“Hii ilani mpya imeweka vipaumbele kwenye masuala ya miundombinu, jambo ambalo linaendelea kutupa matumaini sisi watu wa Kilolo, kwani bado kuna maeneo mengi yanahitaji maendeleo ya barabara na madaraja hii ni ishara kuwa serikali ya CCM bado inaendelea kuwa karibu na wananchi,” alisema Mfalamagoha.

Aidha, alitoa rai kwa wanachama wa CCM kuendelea kuinadi ilani hiyo na kuwahamasisha hata wale walioko upande wa upinzani kuitambua kama nyenzo ya maendeleo kwa Watanzania wote, si kwa ajili ya wanachama wa CCM pekee.

 Alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuunga mkono utekelezaji wa ilani hiyo, kwani inalenga kuboresha maisha ya wananchi wa kada zote, mijini na vijijini.


Ilani hiyo, iliyozinduliwa rasmi tarehe 31 Mei 2025 mjini Dodoma, wakati wa mkutano maalum wa CCM wa siku mbili, imeweka bayana malengo makuu tisa (vipaumbele) ambavyo chama hicho kinakusudia kuyatekeleza katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Vipaumbele hivyo vinajumuisha.


kuwa Ilani inaweka mkazo katika kuongeza thamani ya rasilimali zinazozalishwa nchini kwa njia jumuishi, shindani na fungamanishi,Kuongeza ajira kwa vijana.

Alisema  Ilani hiyo inaelekeza serikali kuzalisha ajira zipatazo milioni 8 katika sekta rasmi na isiyo rasmi kwa kipindi cha miaka mitano, ili kupunguza tatizo sugu la ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu na vijana wengine.


Hata hivyo alisema  Kipaumbele kimewekwa kwenye ujenzi wa barabara, madaraja, reli na usafiri wa anga na maji, hasa maeneo ya vijijini ili kukuza uchumi na kurahisisha maisha ya wananchi,Uimarishaji wa huduma za kijamii.


kuwa  Sekta ya afya, elimu na maji safi na salama zitaendelea kupewa msukumo mkubwa ili kuhakikisha huduma bora zinapatikana kwa wote,Kukuza uchumi wa viwanda.

"CCM inaelekeza kuimarisha sekta ya viwanda kwa kuhakikisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje, pamoja na kujenga viwanda vidogo na vya kati nchini"

Jasmin alisema  kuhusu utawala bora na demokrasia  Ilani hiyo  inaweka wazi dhamira ya kuendeleza mfumo wa kidemokrasia, kuimarisha vyombo vya sheria na kushirikisha wananchi katika maamuzi ya maendeleo,Maendeleo ya vijijini, Kwa kutambua kuwa Watanzania wengi bado wanaishi vijijini, serikali itaelekeza rasilimali nyingi katika kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi wa maeneo hayo kwa wakati,Mageuzi ya kidigitali.

"Ilani inatambua umuhimu wa teknolojia katika uchumi wa kisasa, hivyo serikali itaongeza uwekezaji katika miundombinu ya TEHAMA pamoja na kukuza maarifa ya kidigitali kwa wananchi"


kuwa  Serikali ya CCM itaendelea kuhakikisha nchi inabaki kuwa na utulivu, amani na mshikamano wa kitaifa, kama msingi wa maendeleo endelevu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliwahimiza wanachama wa CCM kuendelea kuwashawishi Watanzania kuunga mkono ilani hiyo na kushirikiana katika kuitekeleza. 

Alisisitiza kuwa ilani hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi na kwamba kila kilichoandikwa ndani yake kinaweza kutekelezeka.

“Tunayo kazi kubwa mbele yetu – kuhakikisha kila Mtanzania anaelewa dhamira ya CCM kupitia ilani hii tutumie kila fursa kuwashawishi watu watuunge mkono na kuungana nasi katika kuitekeleza,” alisema Rais Samia.

Huku mgombea mwenza wa CCM, Emmanuel Nchimbi, pamoja na mgombea wa Zanzibar, Rais Dkt. Husein Ally Mwinyi, walipokea nakala ya ilani hiyo kama ishara ya utayari wao wa kwenda kuinadi nchi nzima wakati wa kampeni zitakapoanza rasmi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani ya CCM, Profesa Kitila Mkumbo, alisema kuwa maandalizi ya ilani hiyo yalizingatia ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wananchi wa kawaida. Aliongeza kuwa lengo kuu ni kuendeleza kasi ya maendeleo yaliyopatikana kwa miaka mitano iliyopita.


Kama ilivyo kawaida, CCM imekuwa chama cha kwanza kuzindua rasmi ilani yake ya uchaguzi kwa mwaka huu wa 2025, hatua inayoashiria maandalizi yake ya mapema kuelekea uchaguzi mkuu.

 Idadi ya wanachama wake imeongezeka na kufikia zaidi ya milioni 13 kupitia mfumo wa usajili wa kidigitali, jambo linaloonyesha uimara na mvuto wa chama hicho kwa Watanzania wengi.

Kwa kumalizia, kada Mfalamagoha alisisitiza kuwa wataalamu na wasomi wana nafasi kubwa ya kusaidia jamii kuelewa kwa kina maana ya ilani na jinsi inavyoweza kubadili maisha ya watu kwa vitendo.

Hivyo  alitoa wito kwa Watanzania wote kuisoma na kuielewa ilani hiyo, kwani ni dira ya maendeleo ya nchi kwa kipindi kijacho.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI