Header Ads Widget

DKT GWAJIMA; KUZENI UNUNUZI ENDELEVU UTAKAO IMARISHA USAWA WA KIJAMII

 


NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Dkt Doroth Gwajima  amezitaka tasisi za ununuzi wa umma kujitahidi kukuza ununuzi Endelevu ambao utaimarisha usawa wa kijamii, maendeleo ya kiuchumi na uendelevu wa kimazingira.

Dkt Gwajima ametoa rai hiyo leo Juni 14 wakati akifungua kongamano la 9 la ununuzi wa umma la mwaka 2025(PPRA) mkoani Arusha kwa niaba ya waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba ambapo amesema kuwa wanapotumia fedha za umma kununua bidhaa, huduma au miradi wanapaswa kufahamu hitaji la maendeleo endevu na ustawi kwa manufaa ya muda mrefu wa wananchi.

"Tanzania kama ambavyo nchi nyingi Duniania imetambua umuhimu wa matumizi ya TEHAMA katika ununuzi wa umma ambapo mifumo hii kwa kiasi kikubwa inaondoa changamoto ya ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele kwenye sekta mbalimbali,"Amesema Dkt Gwajima.

"Tulikuwa tukipishana na magari kupelaka nyaraka, huku huyu hayupo, mara  jaza mafuta yameisha, mzabuni anazusbiri tu,mara umekosea kujaza halafu makaratasi ambayo yangezalishwa yachanwe yachomwe na jambo ambalo lingesababisha athari ya mazingira,"amesema

Ameeleza kuwa Matukizi yamifumo ya kielktriniki yakiendelea kuhamasishwa yana faida kubwa kwa serikali kama ambavyo tumeona NEST imeleta faida mbalimbali ikiwemo kupunguza athari za mazingira na kupungua kwa gharama za kuendesha zabuni za serikali ikiwa ni pamoja na kuondokana na matumizi ya karatasi, kuongezeka kasi ya ununuzi, kupungua makosa katika ununuzi, utuzaji bora wa kumbukumbu na kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

"NEST imeongeza uwazi na  uwajaibikaji, imechangia kuleta thamani  halisi ya fedha inayitumika katika ununuzi lakininpia mfumo huu unaleta faida nyingi na kuimarisha utawala bora pamoja na kuongeza wigo na ushindani  na zaidi  Imesaidia mapambano dhidi ya rushwa, uzembe, udanganyifu na madhaifu katika ununuzi wa umma,"Amesema 

Sambamba  na hayo amesitaka taasisi za manunuzi kuhakikisha matumizi sahihi ya mifumo ya kidijitali katika ununuzi wa umma nchini pamoja na kutetenge asilimia ya ununuzi wao kwa mwaka kwa ajili ya kampuni za wazawa na makundi maalum ili kuhakikisha zabuni zilizotengwa kwa wazawa zinatolewa kwa wazawa kama zilivyokusudiwa.

Aidha ameziagiza halmashauri zote nchini kusaidie kuibua makundi maalum ya kijamii katika maeneo yao ambayo yatajipatia fursa zilizotengwa na serikali kwa ajili yaopamoja na kuwataka wataalam wanaojihisisha na ununuzi kuzigatia weledi wa taaluma zao na maadili.


Kwa upande wake mkurugenzi wa mamalaka ya ununuzi wa umma Denis Simba alisema kuwa mfumo wa NEST ulianza kutumika rasmi Julai 1, 2023 ambapo hadi sasa mfumo una moduli 6 ambazo ni usajili wa watumiaji wa mfumo(e-registration) uchakataji wa zabuni kufanyika katika mfumo (e-tendernet), usimamizi wa mikataba(e-contract) ambayo imekamilika na inatarajiwa kuanza kutumika rasmi Julai, 2025.

"Katika moduli hii zipo moduli nyingine ndo tano ambazo ni uaandaaji wa mikataba, uanzishwaji wa mikataba, utekelezaji wa mikataba, malipo ya mikataba, usitishwaji wa mikataba na mabadiliko ya mikataba, unaona upana wa hii moduli ya e- contract na ndio maana ulituchukua muda kuweza kukamilisha,"Amesema.

"Hapa tunazungumzia ujenzi wa shule darasa moja, ujenzi wa madundu ya vyoo, ununuzi wa bandari,ununuzi unaofanyika kwa wenzetu wa reli, ununuzi wa meli na ununuzi ambao unagusa maeneo mbalimbali," Ameeleza.

Aidha amesema kuwa hadi kufikia Juni 11,2025 wazabuni 38,163 waliidhinishwa na kusajiliwa ambapo kati ya hao 36,377 ni wabuni wa ndani na 1,776 ni wazabuni kutoka nje ya nchi.

Amesema jumla ya taasisi nunuzi 91,415 zikiwemo taasisi kuu za ngazi ya chini za serikali zamitaa zimesajiliwa kupitia mfumo wa NEST zikiwa na jumla ya  watumiaji 131,202 ambao wamesajiliwa NEST. 

Hata hivyo kauli  mbiu ya kongamano hilo ni ununuzi wa umma wa kidigitali kwa maendeleo endelevu, ukuzaji wa kampuni za wazawa na makundi maalum kwa ukuaji wa uchumi jumuishi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI