TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII
Na,Jusline Marco;Arusha
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye msimu mwingine wa maonesho ya karibu Kili- fair mwaka 2025 yanayolenga kuonyesha mnyororo wa thamani katika sekta ya utalii na kuongeza tija kwa watanzania wote.
Akizungumza na waandishi wa habari leo 02 Juni, 2025 wakati akitembelea na kukagua maandalizi ya maonesho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amesema kuwa, Maonesho ya Karibu Kili Fair 2025 yatazinduliwa rasmi Juni 06, na kuhitimishwa Juni 08 mwaka huu katika viwanja vya magereza - Kisongo.
Mhe. Makonda amesema kuwa, zaidi ya makampuni 500 na nchi zaidi ya 40 watakuwa katika viwanja hivyo kubadilishana uzoefu pamoja na kuchochea na kusisimua kwa kiasi kikubwa Utalii huku akiwataka wananchi na Wadau wa Utalii kuchangamkia fursa ya uwepo wa maonesho hayo.
"Karibu Kili - Fair ni fursa kubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha, watanzania na wana Afrika Mashariki, ikilenga zaidi kwenye uchumi, ni jukwaa linalokukutanisha wewe mtoa huduma na mteja wako ili kuhakikisha kuwa mnyororo wa thamani ambao umechagizwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan unaleta tija katika maisha yako". Amesisitiza Mhe. Makonda
Hata hivyo, ametumia fursa hiyo, kuwakaribisha watanzania wote kukaribia Mkoani humo kwasabu kuna fursa nyingi za kutengeneza pesa na kubadilishana uzoefu na wafanyabiashara kutoka mataifa mengine huku akisisitiza watoa huduma wote kwa wageni watakaofika kwenye maonesho hayo kutoa huduma kwa ukarimu ili wageni hao wakaribie tena.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Kili Fair, Dominic Shoo, amesema kuwa maonesho ya mwaka huu yatafanyika kwa viwango vya juu sana na ni tofauti na maonesho yaliyopita kutokana na maboreaho makubwa yaliyofanywa.
Maandalizi ya maonesho hayo yamefikia asilimia 70 na eneo limeongezwa zaidi kutokana na mahitaji ya soko.
0 Comments