Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw Shauri Selenda amefanya ziara kukagua vibali vya uchimbaji wa mchanga kwa magari yote yanayofanya shughuli hizo katika Kata za Mapinga,Kerege,Zinga na Kiromo.
DED Selenda ametoa ushauri na elimu kwa madereva na wamiliki wa magari hayo juu ya
kuhakikisha wanalipa ushuru wa Halmashauri ili kuepuka faini na adhabu mbalimbali
Aidha Mkurugenzi amewasisitiza kuhakikisha wanaendelea kulinda na kutunza mazingira kama ambavyo kauli mbiu inavyotaka "Mazingira yetu na Tanzania ijayo,tuwajibike sasa".
0 Comments