Header Ads Widget

DC CHIKOKA AFUNGUA KONGAMANO LA MADINI NA KUHIMIZA UFATILIAJI WA ELIMU


Na Shomari Binda-Musoma 
MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amefungua kongamano la maonyesho ya ya madini mkoa wa Mara huku akihimiza wachimbaji kufatilia elimu itakayotolewa.

Maonyesho ya madini mkoa wa Mara yameingia katika siku ya pili hii leo juni 4,2025 huku kongamano hilo linalowashirikisha wachimbaji,wauzaji na wachenjuaji likifanyika kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex

Akifungua kongamano hilo Chikoka amesema anaamini palipo na mafanikio kunatikana na kuwa na elimu kama inavyokwenda kutolewa kupitia kongamano hilo.

Amesema washiriki wanapaswa kufatilia kila mada itayotolewa ili kupata uelèwa wa kila jambo litakalofundishwa katika mnyororo mzima wa sekta ya madini

Chikoka amesema kongamano hilo lina umuhimu wa pekee katika kujifunza na kufikia lengo la serikali ya mkoa wa Mara kufikia uchimbaji uchimbaji wenye tija.

Amesema amepata taarifa juu ya mada 5 zinawasilishwa siku ya leo na kuwa na majadilino na kutaka kusikiĺzwa na kujadiliana kwa pamoja.

" Nami leo nimetenga muda ili kwa pamoja tusikilize kwa makini na kuingia kwenye majadiliano ili kuweza kupata uelewa wa pamoja.


" Tusikilize kwa makini na mwisho wa siku baada ya kongamano tutatoka hapa tulipo na kufika mbali zaidi kupitia sekta ya madini", amesema.

Afisa Madini Mkazi mkoa wa Mara Amini Msuya amesema  wayaendelea kufikisha elimu kwa wachimbaji ili mafanikio yaweze kufikiwa.

Msuya zmesema msimamizi wa sekta ya madini atahakikisha suala la elimu linafikia malengo na kuinua kiwango cha uchimbaji.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI