Header Ads Widget

ZANZIBAR KUWAKUTANISHA PAMOJA VIONGOZI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA

NA. THABIT MADAI, ZANZIBAR – MATUKIO DAIMA APP

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa Mara ya kwanza imeandaa Jukwaa maalum la Viongozi  wakuu wa Taasisi za Umma lengo kuimarisha  utendaji na ufanisi Serikalini  pamoja na kukochea ukuaji wa Uchumi wa nchi.

Jukwaa hilo la siku tatu linatarajiwa kufanyika Mei 11 hadi 13 mwaka huu katika ukumbi wa hotel ya Golden Tulip Kiembe samaki mjini Unguja.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Msajili wa Hazina Zanzibar Waheed Ibrahim Mohammed amesema kuwa, Jukwaa hilo la kwanza kufanyika Zanzibar lina lenga kuboresha utendaji wa taasisi za umma na kuleta mafanikio ya kiuchumi na kijamii Zanzibar.

“Jukwaa hili  limetoakana na maono ya Ofisi hiyo pamoja na utekelezaji wa agizo la Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma Tanzania Bara lililofanyika Zanzibar Januari, 2025,” ameeleza.

Ameongeza kuwa,  Wakuu wa taasisi za umma wana majukumu ya uwekezaji kwa umma katika kuendeleza ubora wa huduma, uvumbuzi wa kuongoza na kuchochea ukuaji endelevu wa kiuchumi.

“Mazingira ya kisasa ya kazi, ukuwaji wa Uchumi wa nchi na utendaji uliotukuka unaweza kufikiwa kwa kasi kutokana maono na mashirikiano,” ameeleza.

kiuchumi na kiutendaji yanaendelea kukuwa kwa kasi na  kufikia ubora wa shirika kunahitaji uongozi wenye maono na ushirikiano”, amesema.

Hata hivyo amefafanua kuwa, Jukwaa hilo la kihistoria limelenga kuwakutanisha wakuu wa taasisi za umma na binafsi kutoka sekta mbalimbali ili kubadilishana mawazo, kujadili changamoto zinazofanana katika utekelezaji wa majukumu, kubadilishana uzoefu wa kiuongozi na kuanzisha mikakati ya pamoja ya kuboresha ufanisi na uwajibikaji katika taasisi hizo.

Sanya amefahamisha kuwa Jukwaa hilo litatumika kuwa ni msingi wa ushirikiano wa kimkakati, kukuza mazungumzo kwa kiwango kikubwa, kubadilishana maarifa, kutatua changamoto zilizopo, kufungua fursa na mitandao kati ya viongozi.

Nae Mwenyekiti wa Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma Zanzibar (Zanzibar CEOs Forum) Juma Burhan Mohamed amesema lengo kuu la Jukwaa hilo ni kufikisha huduma kwa wananchi, kutatua changamoto ambazo zinazikumba taasisi za umma pamoja na kutengeneza fursa kwa taasisi binafsi na wananchi kuweza kujua  na kukutana na wakuu wa taasisi za umma.              

Amesema kupitia Jukwaa hilo wataweza kuwaweka pamoja wakuu wa taasisi za umma ili kuwarahisishia wananchi kutatua changamoto zao na kujua fursa zinazopatikana kwa upande wa Serikali na sekta binafsi na kuzifahamu fursa hizo ambazo zitaweza kusaidia kwa lengo la kukuza uchumi wa Zanzibar.

Kwa upande wake CEO wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania Dkt. Said B. Kambi amesema kuwa Taasisi hiyo ipo tayari kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar ili kusaidia kuwajengea uwezo viongozi wa taasisi za umma na binafsi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI