Tanzania inaendelea kuimarika kama ngome ya amani na utulivu barani Afrika chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele kulinda maslahi ya taifa dhidi ya wavamizi wa mawazo na harakati zisizo na nia njema.
Katika mahojiano maalum na Citizen TV ya Kenya, Waziri Kiongozi wa Kenya, Musalia Mudavadi, ameunga mkono kauli ya Rais Samia dhidi ya baadhi ya wanaharakati kutoka nje ya nchi ambao wamekuwa wakijihusisha na mambo ya ndani ya Tanzania kwa namna inayolenga kuvuruga hali ya utulivu.
“Sitaipinga kauli ya Rais Samia kwa sababu kuna ukweli ndani yake... Huko kwetu Kenya uhuru wa maoni umevuka mipaka – hakuna heshima tena,” alisema Mudavadi kwa uwazi mkubwa, akionesha heshima na kuunga mkono msimamo wa Tanzania.
Rais Samia, katika hotuba yake ya hivi karibuni, alitoa tahadhari kuhusu wanaharakati wa kigeni wanaotumia migogoro ya kisiasa kama kichocheo cha vurugu, huku akifichua kwamba baadhi yao walitokea Kenya kwa nia ya kufuatilia kesi ya Tundu Lissu kwa mtazamo wa uchokozi.
“Walishavuruga kwao, tusikubali waje kutuharibia huku. Nchi iliyobaki salama na yenye utulivu ni Tanzania,” alisisitiza Rais Samia.
Kauli hii imepokewa kwa uzito mkubwa na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, ikitafsiriwa kuwa ni ujumbe wa ujasiri na uthabiti wa kulinda uhuru na heshima ya taifa.
Serikali Yaonya: Tanzania Siyo Uwanja wa Majaribio
Serikali imesisitiza kuwa haitavumilia jaribio lolote la kuchochea vurugu kwa kivuli cha harakati au haki za binadamu. Tanzania itaendelea kuwa nchi ya watu wastaarabu, inayothamini amani, utu na mshikamano wa kitaifa.
“Tanzania si uwanja wa majaribio ya fujo na siasa za matusi. Serikali iko imara kulinda amani, utu, na hadhi ya nchi yetu,” imeeleza taarifa rasmi kutoka serikalini.
Katika nyakati ambazo mataifa mengi yanakabiliwa na misukosuko ya kisiasa na kijamii, Tanzania inajitokeza kama mfano wa kuigwa. Uongozi wa Rais Samia unaonekana kuimarisha taasisi za dola, kukuza diplomasia na kulinda maadili ya taifa.
Watu wote wenye nia njema wanakaribishwa kushirikiana na Watanzania kwa kuheshimu sheria na tamaduni za nchi.

0 Comments