Umoja wa Mataifa unasema hakuna msaada wowote ambao umesambazwa huko Gaza licha ya malori ya misaada kuanza kuvuka mpaka baada ya kizuizi cha wiki 11.
Maafisa wa Israel walisema malori 93 yaliingia Gaza siku ya Jumanne, ikiwa na misaada ikiwa ni pamoja na unga, chakula cha watoto, vifaa vya matibabu, na dawa .
Lakini Umoja wa Mataifa ulisema, licha ya malori kufika upande wa Wapalestina wa kivuko cha Kerem Shalom, hakuna msaada wowote ambao umesambazwa hadi sasa.
Msemaji wake Stephane Dujarric alisema timu "ilisubiri saa kadhaa" kwa Israeli kuwaruhusu kufikia eneo hilo lakini "kwa bahati mbaya, hawakuweza kuleta vifaa hivyo kwenye ghala letu".
Israel ilikubali Jumapili kuruhusu "kiasi cha chakula" kuingia Gaza, ambapo wataalamu wa kimataifa wameonya juu ya njaa inayokuja.
Lakini shinikizo la kimataifa kwa Israel limeendelea kukua.
0 Comments