Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu amepandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake mapema mwezi Aprili.
Lissu alikamatwa Aprili 9 baada ya kuitisha mageuzi ya uchaguzi na kuhimiza kususia uchaguzi ujao wa Oktoba.
Anakabiliwa na mashtaka ya uhaini na kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni, ikiwa ni pamoja na madai kwamba alichochea uasi na kuwashutumu polisi kwa utovu wa nidhamu katika uchaguzi.
Hapo awali mahakama ilijaribu kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao, lakini Lissu na timu yake ya wanasheria walipinga hili, wakitaja haja ya uwazi na taratibu zinazostahili.
Kukataa kwake kushiriki katika vikao vya mtandaoni kulisababisha kuonekana kwa ana kwa ana, kufuatia amri ya mahakama.
Uwepo mkubwa wa polisi haujawazuia wafuasi, ambao wengi wao wamekusanyika nje ya mahakama.
Ufuatiliaji wa yanayojiri kimataifa umeongezeka, hasa baada ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Martha Karua kunyimwa kuingia Tanzania kuhudhuria kikao hicho.
Karua, akiongoza kampeni ya haki za Afrika nzima, alilaani mamlaka za Tanzania kwa vitendo vyao na kutoa wito kwa vyombo vya kikanda kuiwajibisha serikali.
Pia kuna ripoti kwamba jaji mkuu mstaafu wa Kenya na rais wa Mahakama ya Juu Willy Mutunga amezuiliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Huku mwenendo wa kesi mahakamani ukiendelea, hali inaendelea kuwa tete, huku jumuiya ya kimataifa ikifuatilia kwa karibu maendeleo na dhamira ya serikali ya Tanzania katika kanuni za kidemokrasia zinazochunguzwa.
Lissu alipanda kizimbani akionekana mwenye furaha na bashasha , alipata nafasi ya kusalimia watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama chake.
Amelaani pia kuzuiwa kwa aliyekua Jaji mkuu wa Kenya Willy Mutunga uwanja wa ndege ili asiweze kuhudhuria kesi hiyo.
''Kama mnaweza kumrudisha jaji Mkuu Willy Mutunga Airport, asije kuangalia kesi inaendaje, mmekwisha''. Alisema Lissu.
MWISHO.
0 Comments