Tangazo la Joe Biden kwamba amepatikana na saratani ya tezi dume limefufua maswali kuhusu masuala ya kiafya ambayo rais huyo wa zamani wa Marekani alikuwa akikabiliana nayo alipokuwa katika Ikulu ya White House.
Katika taarifa ya Jumapili, ofisi ya Biden ilisema mzee huyo wa miaka 82 alipata alibainika kuwa na maradhi hayo siku ya Ijumaa baada ya kuonana na daktari kutokana na dalili zilizojionesha za njia ya mkojo.
Baadhi ya madaktari wameeleza kushangazwa na aina hiyo kali ya saratani, ambayo imesambaa hadi kwenye mifupa yake, haikugunduliwa mapema.
Wengine walisema kwamba saratani zinaweza kukua haraka bila mgonjwa kuonesha dalili, na kwamba wanaume zaidi ya 70 hawachunguzwi mara kwa mara.
Rais Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba mtangulizi wake alipaswa kuwa wazi zaidi kwa umma, akionekana kuashiria kuwa utambuzi wa saratani ulikuwa umefichwa, kauli iliyokanushwa na msaidizi wa Biden.
0 Comments