Header Ads Widget

THRDC YAWATAKA WANACHAMA WAKE KUSOMA NA KUZIELEWA KANUNI ZA UCHAGUZI KABLA YA KUOMBA VIBALI VY KUWA WAANGALIZI

 


NA NAMNYAKI KIVUYO ARUSHA

Mkurugenzi wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC)Onesmo Ole Ngurumwa amtoa angalizo kwa Asasi za kiraia na wasaidizi  wa kisheria kupitia na kuelewa kanuni za uchaguzi kabla ya kuomba vibali vya kuwa waangalizi kutokana na kanuni hizo kuwazuia kusema jambo lolote wakati wa uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Ole Ngurumwa ameyasema hayo  wakati akifungua mafunzo kwa wasaidizi wa kisheria kutoka asasi mbalimbali za kiraia ambapo alisema kuwa kanuni hizo zina changamoto nyingi ambazo zitawafanya waangalizi kujinyima haki zao zote kama watetezi wa haki za binadamu mpaka uchaguzi utakapoisha.

"Hamtaweza kuongea chochote, hamtaweza kushauri chochote na ikitokea umekiuka kanuni hizo unaweza ukafungiwa kufanya kazi za NGO'S kwa maisha yako yote na hata kufungwa jela," Alisema Ole Ngurumwa. 

Amefafanua kuwa kanuni hizo zimetungwa na tume wenyewe kwani wamepewa mamlaka hayo kwahiyo wanapaswa kuwaomba waangalie namna ya kuzilegeza kwasababu Asasi  za kirai zikifanya kosa kwenye  kanuni hiyo hakuna nafasi ya kusikilizwa bali adhabu itatolewa moja kwa moja na hakuna pa kukata rufaa na hiyo ni sheria kali sana na hatujawahi kuwa na sheria yenye kifungu ambachi adhabu yake haina  kikomo zaidi ya hii.


"Kwa wanachama wetu msije mkaingia hutaweza  kichwa kichwa kama mtataka labda tuwaombee lakini sijui kama itawezalekana kwasababu kuna changamoto ya kutokukubali kukutana na wadau na barua hawajibu kwahiyo yoyote mwenye nia ya kuwa mwangalizi wa uchaguzi soma kwanza hizo kanuniusije ukalitumbukiza shirika lako kwenye changamoto ambayo usiyoweza kutoka au kujikuta wakati wote wa uchaguzi umefungwa mdomo,"alieleza.

"Yaani hata uone tatizo kubwa kiasi gani hutaweza kuzungumza tofauti na miaka ya nyuma ambapo tulikuwa na uwezo wa kuongea tulivyokuwa tunafuatilia uchaguzi kila wiki tulikuwa tukitoa  taarifa, hali ikoje na tunatoa ushauri na vilikuwa vinafanyiwa kazi sasa sijui wakati huu kanuni inakunyima kufanya chochote hata kama nj tatizo dogo kiasi gani,"aliendelea kusema.

"Utasubiri uchaguzi uishe, uandike ripoti yako na kabla hujaitoa uipeleke tume na wao ndo watakuruhusu kuitoa, sasa hiyo kwa mtetezi halisi anayejua haki zake huko ni kusalimisha haki zake na kugeuka kuwa mtumishi wa tume,"

"Hatupaswi kuwa watazamaji japo wametuita watazamaji kwasababu NGO yoyote ya Tanzania haipaswi kuwa mtazamaji unatazama nini kwenye nchi yako? Unatakiwa uwe mwangalizi na ukiona kuna tatizo lolote uchukue hatua ikiwemo kutoa taarifa ili iwafikie tume na waweze kutatua,"

" Sisi ni watu wa Tanzania na uchaguzi nu wakwetu, tulizani tuna nafasi kubwa ya kushauri pale tunapoona changamoto zinajitokeza kwahiyo hizo kanuni angalau kama tukiweza kuongea na Tume waweze kubadisha hasa vifungu vyenye changamoto,"

Sambamba na hayo amezitaka Asasi hizo kuzingatia utoaji wa taarifa ikiwa ni pamoja na kutafiti na kuwa na mikakati ya msingi ya utetezi wa haki za binadamu kwani haitakiwi nguvu wakati wote bali mikakati na ushawishi

Pia amewataka kuanza kuenenda na teknolojia ikiwemo matumizi ya Akili mnemba(AI) ili kuweza kuzifaidi na kupunguza ghara mojawapo ikiwa ni kuacha matumizi ya karatasi.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo Abdulahi Rugome ambaye ni mkurugenzi wa shirika la TUNAWEZA alisema kuwa kanuni zilizotolewa na Tume huru ya uchaguzi Tanzania zinawabana na zinawafanya wawe kama Mbweha.



"Mbweha ni yule mnyama ambaye anakimbia kimbia tu porini pasina kujitetea kwahiyo tutashindwa sisi watetezi wa haki za kibinadamu kwanza kujitetea wenywewe lakini pia kuitetea jamii hivyo naishauri tume pamoja na serikali kuweza kukaa pamoja na kuziangalia kanuni hizi na wawashirikishe pia wadau," Alisema Abdulahi.

Naye Mkurugenzi wa shirika la Wezesha mwanamke Happy Fransis alisema kuwa mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka na yatawasaidia wao kama watetezi kuweza kujilinda na kuwa salama hasa kwa kipindi hiki nchu inanapoelekea katika uchaguzi mkuu.

" Yatatusaidia namna ya kuenenda kama watetezi kwaajili ya usalama wetu na hata kwaajili ya usalama ya wale ambao tunawafanyia utetezi,"Alisema.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI