Header Ads Widget

THRDC YAANZA KUTOA MAFUNZO MAALUMU YA UFUATILIAJI NA UTOAJI WA TAARIFA ZA MATUKIO YA HAKI ZA BINADAMU KWA WATETEZI WA NGAZI YA JAMII

NA MATUKIO DAIMA MEDIA ,ARUSHA 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeanza mafunzo maalumu ya siku mbili kwa Watetezi wa Haki za Binadamu kutoka ngazi ya jamii pamoja na Waratibu wa Kanda wa mtandao huo. 

Mafunzo haya yanafanyika mkoani Arusha kuanzia tarehe 8 hadi 9 Mei 2025, yakilenga kuwaongezea ujuzi kuhusu mbinu bora za ufuatiliaji na utoaji wa taarifa za matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu.


Mafunzo haya yamewakutanisha zaidi ya watetezi 70 kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Pwani, Mashariki na Kanda ya Kati, ambao wanatetea haki mbalimbali zikiwemo haki za watoto, wanawake, mazingira, waandishi wa habari, wafugaji, watu wenye ulemavu, pamoja na haki za kiraia na utawala bora.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa, alieleza kuwa watetezi wa haki kutoka ngazi ya jamii ni nguzo muhimu katika kujenga jamii salama inayoheshimu na kulinda haki za binadamu kuanzia ngazi ya chini hadi kitaifa.


Wakili Olengurumwa aliongeza kuwa moja ya majukumu muhimu ya watetezi wa haki za binadamu ni kutoa taarifa sahihi kuhusu hali ya haki za binadamu kwa jamii, viongozi, vyombo vya habari na wadau mbalimbali ili kusaidia kuimarisha mazingira ya haki nchini. 

Hivyo, elimu kuhusu mbinu za kufuatilia na kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki ni msingi muhimu wa kazi yao.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI