Awali wafanyabiashara wa Tanzania waliagizwa kusitisha usafirishaji wote kwenda Afrika Kusini na Malawi
Tanzania na Malawi wamekubaliana kuandaa taratibu za uendeshaji wa bidhaa za kilimo hususani kuhusu afya ya mimea, pamoja na hatua zingine za kiutawala zitakazoimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano kati ya mawaziri wa mambo ya nje na wa kilimo wa nchi hizo mbili, uliofanyika katika Dodoma, Tanzania siku ya Ijumaa, tarehe 2 Mei.
Mkutano huo ulifuatia kuondolewa kwa marufuku ya uagizaji na usafirishaji wa bidhaa za kilimo kati ya nchi hizo mbili. Marufuku hiyo ilisababisha mvutano wa kibiashara, ambapo Tanzania ilienda mbali hata kuizuia Malawi kutumia bandari ya Dar es Salaam.
“Timu zote mbili zinatambua uhusiano wa kihistoria na wa kindugu pamoja na urafiki wa karibu uliodumu kwa muda mrefu kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Malawi,” inasomeka sehemu ya taarifa ya mkutano huo
Mnamo mwezi Machi, Malawi iliweka marufuku ya uingizwaji wa baadhi ya mazao kutoka nchi zote, ikisema ilikuwa ni hatua ya muda kwa bidhaa kutoka nchi zote ili kuwalinda wazalishaji wa ndani.
Tanzania ilikosoa hatua ya Malawi, ikisema iliwaathiri moja kwa moja wafanyabiashara wa Tanzania na kueleza vizuizi hivyo kuwa "visivyo vya haki na vyenye madhara."
Katika taarifa yao, ujumbe huo ulieleza kuthamini umuhimu wa kuimarisha na kuendeleza ushirikiano wa pande mbili kwa manufaa ya nchi zote mbili.
0 Comments