Header Ads Widget

SMAUJATA MARA YAINGIA SIKU YA PILI KUTOA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA SHULE ZA MUSOMA


Na Shomari Binda-Musoma 

ELIMU ya masuala ya ukatili wa kijinsia na masuala ya maadili kwa wanafunzi imeendelea kutolewa na viongozi wa Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii ( SMAUJATA)mkoa wa Mara kwa kushirikiana na viongozi wa Wilaya ya Musoma.

Wazazi na wanafunzi wa shule ya msingi Songambele leo mei 30,2025 wamefikishiwa elimu hiyo na SMAUJATA kwa kuwezeshwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Musoma kupitia Katibu Tawala Ally Mwenda.

Awali akizungumza kwenue kikao cha wazazi wa shule ya Songambele Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Mara Joyce James Ngasa amesema wazazi wasiwaache watoto kujilea wenyewe majumbani.


Amesema malezi yanaanzia nyumbani kwa uangalizi mzuri wa watoto na kazi ya kulea wasiachiwe walimu pekee yao.

Joyce amesema kwa sasa mmomonyoko wa maadili umekuwa mkubwa na ndiuo iliyopelekea SMAUJATA mkoa wa Mara na Wilaya ya Musoma kupita mashuleni kutoa elimu

Amesema wazazi wanapaswa kutimiza wajibu wao kwa kuzungumza na watoto na kuwaelekeza maadili mema na kutowafanyia ukatili wa aina yoyote.

Baada ya kuzungumza na wazazi Mwenyekiti huyo alizungumza na na wanafunzi wa shule ya msingi Songambele na kuwataka kutoa taarifa pale wanapofanyiwa vitendo vya ukatili vikiwemo vya ubakaji na ulawiti.


Amewaambia wanafunzi hao pale wanapofanyiwa vitendo vibaya kutoka kwa mtu yoyote ikiwa nyumbani au sehemu yoyote watoe taarifa.

" leo tumeendelwa na utoaji wa elimu kwa kufika shule ya msingi Songambele na kuzungumza na wazazi pamoja na wanafunzi.

" Tumepokelewa vizuri na uongozi wa shule na tumewaelekeza wazazi juu ya kujiepusha na ukatili wa aina yoyote kwa watoto lakini pia tumezungimza na wanafunzi tunaamini kampeni na elimu hii italeta mabadiliko",amesema.

Aidha Mwenyekiti hiyo wa SMAUJATA mkoa wa Mara ameushukuru uongozi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuwapa ushirikiano na kuwawezesha usafiri wa kufika mashuleni na kutoa elimu.

Kampeni ya utoaji elimu unaofanywa na SMAUJATA mkoa wa Mara inaendelea kwenye shule za msingi na sekondari Wilaya ya Musoma na baadae itaendelea kwenye Wilaya nyingine za mkoa wa Mara.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI