Na Shomari Binda-Musoma
KAMPENI ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii( SMAUJATA) mkoa wa Mara imeanza ziara ya kupita kwenye shule za mzingi na sekondari ikiwa na lengo la kutoa elimu.
Elimu inayotolewa ni masuala ya ukatili wa kijinsi,namna ya utoaji wa taarifa kwa watoto wanaofanyiwa vitendo hivyo na uhimizaji wa maadili mema.
Katika siku ya kwanza mei,28,2025 kampeni hiyo imefika shule ya msingi Kambarage A na B na kufikisha elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Akiwa shuleni hapo Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Mara Joyce James Ngasa alitoa mada kujusiana na mitandao salama kwa watoto na kuwaeleza wanafunzi wanapotumia simu za wazazi na walezi watumie kwa kupata elimu na sio mambo yasiyofaa.
Amesema mirandao isiyo salama inachangia mmomonyoko wa maadili na kuzalisha kizazi kisichofaa.
Joyce amesema yapo mambo mazuri yanayofaa kwenye mitandao wanayopaswa wanafunzi kuyatumia.
" Tunawashukuru walimu kwa kutupokea vizuri shuleni hapa na tumekuja kutoa elimu kwa wanafunzi kwa masuala mbalimbali yakiwemo ya maadili mema kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na matumizi mazuri ya mitandao."Nimekuja na wenzangu
Mwenyekiti wa Idara ya Uenezi na Uanachama mkoa shujaa Masatu Robert pamoja na mkuu wa idara ya elimu mkoa shujaa Lena Enock kwa kutambua uzalendo na umuhimu wa Taifa letu tumefika shule za msingi Kambarage A/B zilizopo kata ya Bweri Wilaya Musoma ili tutoe elimu ya Ukatili wa kijinsia,mmomonyoko wa maadili na Mtandao salama kwa mtoto.
Mwenyekiti huyo amemshukuru Katibu Tawala wa Wilaya ya Musoma Ally Mwendo kwa kuwezesha usafiri unaosaidia kufanya kampeni hiyo kwa kufika mashuleni
Kwa upande wao walimu wa shule hozo wamependezwa na kampeni hoyo na kazi inayofanywa na mashujaa wa SMAUJATA mkoa wa Mara na kuomba kujiunga nao.
0 Comments