Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Serikali imepeleka Zaidi ya shilingi Milioni 700 kwa ajili ya upanuzi wa kituo Cha Afya Wanging'ombe mkoani Njombe kinachohudumia Takribani Wakazi Elfu 20220 na kutibu wagonjwa 13500 kwa mwezi.
Dr Francis Hoya ni Mganga mfawidhi wa kituo hicho ambaye anasema Hadi sasa zimetumika Zaidi ya shilingi Milioni 200 na wanaendelea na upanuzi.
Mbunge wa Jimbo la Wanging'ombe Dokta Festo Dugange Naibu Waziri wa Tamisemi amesema atahakikisha Vifaa tiba pia vinapelekwa katika kituo hicho ambacho ni muhimu katika ustawi wa Afya za wananchi wake.
Awali mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Zakaria Mwansasu amesema Miradi yenye Thamani ya shilingi bilioni 2.84 inapitiwa na Mwenge wa uhuru 2025.
Kwa upande wake mkimbiza Mwenge wa uhuru Kitaifa Mwaka huu Ismail Ali Ussi ameridhika na upanuzi wa kituo hicho huku akisisitiza wataalamu kuwahudumia wananchi kwa weledi mkubwa.
Baadhi ya wakazi wa Wanging'ombe akiwemo Sanford Danda wameonesha furaha yao juu ya kujengwa na kuendelea kupanuliwa kwa kituo hicho na kwamba kinawasaidia sana kupata huduma za Afya.
0 Comments