Na Hadija Omary Matukio Daima Media
Mwenge wa Uhuru ukiwa unaenda na mbio zake Mkoani Lindi Leo utakimbizwa Wilayani Kilwa ukitokea Wilayani Liwale ambapo utaona, utazindua na kuweka Mawe ya Msingi Katika miradi 13 ya Maendeleo yenyethani ya zaidi ya shilingi Bilioni 11
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mohamed Nyundo akizungumza wakati wa mapokezi ya mwenge huo yaliyofanyika Katika kijiji cha zinga kikaoni amesema mwenge wa huru ukiwa Wilayani humo utakimbizwa umbali wa kilometa 173
Hata hivyo nyundo alisema kuwa Kati ya miradi hiyo 13 itakayopitiwa na mwenge wa huru miradi 10 itaonwa, miwili itawekwa Mawe ya Msingi na Mmoja utazindua
kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Ismail ally usi amesisitiza kuwepo na taarifa sahihi Katika miradi husika vifaa kuhakiki miradi inapoitajika pamoja na wataalamu
Hata hivyo aliwataka wananchi kuhusianisha mwenge wa Uhuru na itikadi za kisiasa na kwamba dhamira ya mwenge huo toka ulipo asisiwa ulikusudia kuchochea Maendeleo, Amani na upendo huku ukijikita kuondoa chuki na dharau
0 Comments