Header Ads Widget

MBUNGE ZUENA HAPOI ENDELEZA KAMPENI YA KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKATIBU UWT WILAYA.

 


Na WILLIUM PAUL, SIHA. 


MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri ameendelea na kampeni yake ya kuhakikisha nyumba za Makatibu wa Umoja wa Wanawake wilaya katika mkoa wa Kilimanjaro zinakamilika ambapo amegawa mabati 50 kwa wilaya ya Siha na Hai. 


Zoezi hili linafanya Mbunge huyo kutoa mabati kwa wilaya hizo mbili linafanya kutimiza adhima yake ya kugawa mabati kwa wilaya saba za mkoa huo. 



Akizungumza wakati anakabidhi, Zuena alisema kuwa lengo lake ni kuhakikisha nyumba hizo zinakamilika na kuweka mazingira safi na rafiki kwa Makatibu hao kutekeleza wajibu wao. 



Katika hatua nyingine Mbunge huyo alisema kuwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika mkoa wa Kilimanjaro na kuwataka wakinamama kutoka kifua mbele na kuisemea miradi hiyo kwa wananchi. 



"Wakinamama tunapaswa kuwa mstari wa mbele katika kueleza kazi zote zilizofanywa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani zinaonekana wazi kwa macho ya nyama hakuna tunachomdai sisi wana Kilimanjaro bali yeye ndio anatudai tunapaswa kumlipa kwenye boksi la kura Oktoba mwaka huu" Alisema Mbunge Zuena. 


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI