Header Ads Widget

MAANDALIZI YA MKUTANO MAALUM WA CCM TAIFA YAKAMILIKA DODOMA

 

Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima Media Dodoma 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema maandalizi ya Mkutano Maalum wa Taifa yamekamilika kwa kiasi asilimia 100 huku mkutano huo ikitarajiwa kuandika historia mpya katika uendeshaji na mwelekeo wa chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.


Akizungumza  leo Mei 24 2025, jijini Dodoma, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, amesema ratiba ya mikutano hiyo inaanza Mei 26 kwa kikao cha Kamati Kuu, kikiendelea Mei 28 kwa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kabla ya Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa unaotarajiwa kufanyika Mei 29 na 30.


Ajenda kuu za mikutano hiyo ni pamoja na kupokea taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, uzinduzi wa Ilani mpya ya uchaguzi kwa pande zote mbili, marekebisho ya Katiba ya Chama pamoja na tukio la uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya jengo jipya la Makao Makuu ya CCM.


Jengo hilo jipya linatarajiwa kuwa la kisasa na lenye uwezo mkubwa wa kuhudumia wanachama na shughuli za chama, likiwa na kumbi za mikutano na maegesho ya magari, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya muda mrefu ya CCM katika kujenga miundombinu imara inayoendana na ukuaji wa chama.


"CCM ina wanachama zaidi ya milioni 11 nchini na idadi hiyo inaendelea kuongezeka kila siku, hali inayodai ongezeko la uwezo wa kimfumo na kimuundo katika ngazi zote za chama,"Amesema SPA Makalla.


Hata hivyo amesema Wajumbe zaidi ya 2,000 wa Mkutano Mkuu wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo kwa mujibu wa Katiba ya chama, huku wanachama na wananchi wakihimizwa kufuatilia shughuli hizo kupitia televisheni na mitandao ya kijamii.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI