Na Gabriel Kilamlya Matukio Daima Media NJOMBE
Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Shukrani Kawogo amewataka wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani humo kujitokeza katika Matawi na kuchukua Kadi zao za Kielektroniki kupitia makatibu Tawi waliko jisajili.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mwenezi huyo amesema CCM wilayani humo kimepokea Kadi za Kielektroniki zipatazo Elfu 48 na zinatarajiwa kuanza kugawiwa Mei 22 mwaka huu.
Aidha ameeleza kuwa watahakikisha wilaya nzima inapata kadi hizo ambazo zilisubiriwa kwa hamu kubwa na wanachama wa CCM hivyo zoezi la ugawaji litafanyika kwa weledi mkubwa katika matawi yote.
Sanjali na hilo pia amesisitiza kuwa Kadi hizo hutolewa bure pasipo malipo ya aina yoyote bali mwanachama anachotakiwa kwenda nacho ni kitambulisho cha Nida sambamba na kitambulisho cha Mpiga kura ili kuwezesha uhakiki wa taarifa zilizopo kwenye vitambulisho hivyo na Kadi ya uanachama.
Ameongeza kuwa zoezi hilo linawahusu wanachama wote waliosajiliwa katika mfumo bila kujali kama awali alipata Kadi ya Kielektroniki kwani Kadi za sasa zimeboreshwa hivyo wote watapatiwa upya.
" Kuna wale wanachama ambao miaka ya nyuma walipata Kadi za Kielektroniki, katika zoezi hili la sasa nao pia ni walengwa kwani Kadi za sasa zimeborezwa zaidi ukilinganisha na zile za awali hivyo nao wafike ili waweze kupatiwa Kadi mpya".
0 Comments