Header Ads Widget

JUMUIYA YA WAZAZI MARA YASISITIZA USIMAMIZI WA MAADILI KWA WATOTO


Na Shomari Binda-Rorya

JUMUIYA ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) mkoa wa Mara imesisitiza maadili mazuri kwa watoto ikiwemo usimamizi mzuri wa malezi kutokana na kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili.

Msisitizo huo umetolewa leo mei 16,2025 na Katibu wa jumuiya hiyo mkoa wa Mara Baraka Mwachula katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kutembelea wilaya za mkoa huo kukagua uhai wa jumuiya na chama na masuala mengine.

Akizungumza na Kamati za Utekeleza za Kata wilayani Rorya licha ya mambo mengine amesema suala la maadili ya watoto lina umuhimu mkubwa na kila mmoja anapaswa kulisimamia.

Amesema mmomonyoko umekuwa mkubwa kwenye jamii na bila kuliangalia na kusimamia hali itakuwa mbaya zaidi.


Baraka amesema jumuiya ya wazazi moja ya majukumu yake ni kusimamia malezi na maadili hivyo kila kiongozi na mwanacha atekeleze majukumu hayo.

" Ndugu zangu wana Rorya leo ni siku ya kwanza ya ziara yangu wilaya za mkoa wa Mara na nimeanzia hapa wilayani Rorya na nimeona nianze na hilo la maadili kwa watoto wetu.

" Twendeni tukasimamie maadili ya watoto wetu kutokana na kuzidi kualibikiwa na sisi kama wazazi hatupaswi kuona hali hiyo ikiendelea",amesema.

Licha ya kuzungumzia maadili katibu huyo amewaasa viongozi hao wa jumuiya ya wazazi wilayani Rorya katika kuelekea uchaguzi mkuu amewataka kuwa makini na watakaojitokeza kugombea.

Amesema wapo wengi watajitokeza lakini ni muhimu kuangalia watakaoweza kuwasaidia na kujiandaa kuwachagua viongozi watakaofaa.

" Nisisitize muda ukifika tuangalie mgombea sahihi atakayeweza kutuvusha na tukawashawishi wale wanaofaa waweze kugombea na akijitokeza mgombea kutoka kwenye jumuiya yetu tumuunge mkono.

" Tukashiriki kampeni muda ukifika kuhakikisha Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo kwa kuwa yale aliyoyafanya Mama Samia yanaonekana.

Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Jumuiya hiyo mkoa wa Mara Vicent Eunyo amesema ili kuimalisha jumuiya na chama ni muhimu kulipa ada na viongozi kuhakikisha wanafanya ziara kuanzia ngazi ya mashina hadi wilaya kama ambavyo mkoa wanafanya.

Kuelekea uchanguzi unaokuja ndani ya chama amesema viongozi wa jumuiya na chama wanapaswa kuwa watulivu na kujiepusha na viongozi watakaotaka kugombea kwa kutanguliza Rushwa.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Rorya Venance Magege amesema wamepokea maelekezo ya Katibu wa mkoa ikiwa ni pamoja na maelekezo ya kufanya ziara na wanakwenda kufanyia kazi.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI