Header Ads Widget

HABARI KUBWA KWA WANAHABARI UZINDUZI WA MRADI MPYA WA KUWAJENGEA UWEZO WA WANAHABARI ILI JAMII IWEZE KUPATA TAARIFA SAHIHI

 


 NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

“Empowering Journalists for Informed Society”

Leo jijini Dar es Salaam, IMS kwa kushirikiana na UTPC na JamiiAfrica wamezindua rasmi mradi mpya wa miaka mitatu unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Serikali ya Uswisi (SDC). 

Mradi huu, utakaotekelezwa kuanzia mwaka 2025 hadi 2027, unalenga kuwawezesha waandishi wa habari ili jamii iweze kuwa na uelewa mpana kupitia taarifa sahihi.

Uzinduzi huu umeambatana na mijadala mbalimbali muhimu iliyoendeshwa na wanahabari wabobezi ikiwemo:

 "Uandishi wa Habari ni Muhimu Kuliko Wakati Wowote" na athari za zama za kidijitali katika umuhimu wa uandishi wa habari nchini Tanzania.

Bi. Imani Luvanga alisisitiza kuwa taasisi za kihabari hapa nchini zinapaswa kufanya jitihada kubwa kuwalinda wanahabari  ili waweze kufanya kazi kwa uhuru zaidi, lakini pia kuhakikisha mafunzo yanayotelewa yanawafikia wale walio na ari ya kujifunza, na kwa kutumia wakufunzi ambao ni wanahabari halisi ili kujenga uaminifu.


Mkurugenzi wa UTPC, Kenneth Simbaya, alisema kuwa mradi huu unaoangazia sauti za jamii kusikika kupitia waandishi wa habari, unaweza kuibua taarifa ambazo hazitapendelewa na kila mtu.

 Hata hivyo, uzoefu wa taasisi kama UTPC unaonyesha kuwa changamoto hizo zinaweza kutatuliwa kwa kufanya majadiliano na serikali ili kueleza faida ya kuwa na vyombo huru vya habari.

Naye Mkurugenzi wa JamiiAfrica Maxence Melo alibainisha kuwa mradi huu hauhusiani na uchaguzi  wala haujaanzishwa kwa ajili ya uchaguzi, bali ni wa muda mrefu ambao utakuwepo  kabla ya uchaguzi, wakati na baada ya uchaguzi.

 Lengo ni kuwajengea wanahabari uwezo wa kutumia teknolojia kubaini taarifa potofu.

 JamiiAfrica imeweka mifumo imara ya ushirikiano na taasisi kama UTPC na LHRC ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi huu unaleta matokeo.

Katika hotuba yake, Mkurugenzi wa IMS, Jasper Højberg, alisema kuwa ushirikiano ni nguzo muhimu katika kukuza tasnia ya habari, hasa wakati huu ambapo changamoto ya rasilimali ni kubwa. 

Alieleza kuwa IMS inaendelea kuhimiza mbinu mpya za kibiashara ili vyombo vya habari viweze kujitegemea na kustawi.


TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

Naye ,Mwakilishi wa EU, Bi. Isabelle Mignucci, alisema kuwa mradi huu unalenga kujenga mazingira bora ya habari ambapo kila sauti inasikika na kila raia anapata taarifa sahihi na za kuaminika. 

Aliongeza kuwa vyombo vya habari ni nguzo muhimu ya demokrasia na uwajibikaji, na mradi huu unaangazia hasa vijana, wanawake na jamii za vijijini.


Bw. Holger Tausch kutoka SDC aliishukuru UTPC kwa kazi kubwa ya kufuatilia na kurekodi madhila yanayowapata waandishi wa habari na kuonyesha ukubwa wa tatizo, na alishukuru pia kwa midahalo ya ulinzi na usalama iliyofanyika kati ya waandishi wa habari na Jeshi la Polisi ambayo imeimarisha mahusiano kwa kiasi kikubwa. 

Alisema kuwa sekta ya habari Tanzania baro ina changamoto licha ya hatua zilizopigwa kwenye ripoti ya World Press Freedom Index, hivyo na ni muhimu kuendelea kuzifanyia kazi changamoto hizo na kwamba serikali ya Uswizi itaendelea kutoa ushirikiano kwa sekta ya habari Tanzania.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI