Header Ads Widget

FLAVIANA MATATA FOUNDATION YAWANOA WANAHABARI


Na Fatma Ally Matukio DaimaApp

Waandishi wa habari nchini Tanzania wametakiwa kuyaibua matukio ya ukatili wa kijinsia wanayotendewa hususani watoto wadogo kwa kuzingatia sheria, kanuni za uandishi wa habari ili kuepusha upotoshaji na ukandamizaji.

Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Rehema Longo ambae ni mwezeshaji wa stadi za maisha kitaifa wakati akiwajengea uwezo waandishi kuhusu namna bora ya kuyaripoti matukio ya ukatili wa kijinsia .

Amesema kuwa, wanaishukuru FLaviana Matata Foundation (FMF), chini ya ufadhili wa Women fund Trust (WFT) kwa kuona umuhimu wa kuisaidia Serikali kuelimisha watu kuhusu stadi za maisha.

"Leo tumekutana na waandishi wa habari wamejifunza mambo mengi kuhusu jinsi na jinsia, Afya ya uzazi pamoja na stadi za maisha zinazosaidia sana vijana hata Jamii, mtu anaweza kujitambua,"

"Stadi za maisha zitasaidia sana kizazi chetu kuweza kubadilika, waandishi mukawe mabalozi wazuri,mafunzo haya tuliyoyapata leo yakatuenue kuweza kuripoti vizuri matukio haya"

Kwa upande wake, Afisa Miradi kutoka Taasisi  ya FLaviana Matata Foundation (FMF) Suzan Cleophas amesema kuwa ili kuhakikisha watoto wanapata elimu wameanzisha mradi wa "Afya yangu, Haki yangu"ambao utafanyika kwa miaka mitano.


Amesema kuwa, lengo kubwa la mafunzo hayo kwa waandishi wa habari ni kuwajengea uwezo na kuwapatia elimu ya Afya ya uzazi na ukatili wa kijinsia kupitia mradi huo uliofadhiliwa na Women fund Trust ambao ndio wadau wakubwa.

Amesema kuwa, mradi huo umeanza kufanya kazi mwaka jana ambapo wameanzia pwani kwa kukutana na wanafunzi wa shule ya Msata na Kiwangwa, pia wametembea baadhi ya vyombo vya habari ndipo wakaona kuna umuhimu  mkubwa wa kukutana waandishi wa habari kuwajengea uwezo wa kuripoti matukio ya ukatili.

Ameongeza kuwa, kazi zao wanafanya kwa ukaribu mkubwa na Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Elimu, huku wakishirikiana na Mkoa wa Shinyanga, Njombe,Pwani, Ruvuma pamoja Mwanza ambapo wamechagua mikoa hiyo kutokana takwimu za Serikali zilizotolewa juu ya  matukio ya ukatili.

"Na tunaendelea kutoa elimu kw jamii kwa kuyafukia makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi wakiume, waandishi wa habari, kutokana mpango mkakati wetu mradi huu ni wa miaka 5 umeanza mwaka 2023 hadi 2027 lengo la kuyaondoa kabisa Matukio haya ya ukatili"amesema Suzan

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI