Sean "Diddy" Combs anadaiwa kutumia nyundo kujaribu kuvunja nyumba ya mpenzi wake wa zamani baada ya kushambuliwa katika hoteli ya Intercontinental mnamo 2016, mahakama ya New York imeelezwa.
Video ya usalama ya Bw Combs ya kushambuliwa kwa mpenzi wake wakati huo Casandra "Cassie" Ventura imeoneshwa mahakamani mara kadhaa katika kesi yake ya ulanguzi wa ngono.
Rafiki mkubwa wa zamani wa Bi Ventura Kerry Morgan Jumatatu alisimulia jinsi Bw Combs alivyojaribu kubomoa nyumba ya Ventura baada ya tukio hilo, na akaeleza kisa hicho kuwa cha kuogofya.
Bw.Combs, 55, amekana mashtaka ya ulaghai, ulanguzi wa ngono na usafirishaji ili kujihusisha na ukahaba. Anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha jela ikiwa atapatikana na hatia.
Bi.Morgan aliiambia mahakama kuwa alikuwa katika nyumba ya Bi Ventura ya Los Angeles baada ya tukio la hoteli na alitazama kupitia tundu huku Bw Combs "akigonga mlango kwa nyundo".
Bi.Morgan aliiambia mahakama kwamba ilipotokea, hakufikiri kwamba Bi Ventura hakujali iwapo Bw Combs "aliingia na kumuua".
Bw.Combs hakuingia ndani ya nyumba hiyo na maafisa wa polisi walifika kama saa tatu baadaye, Bi Morgan alisema. Hakuna malalamiko yaliyowasilishwa.
Mahakama ilisikiliza madai zaidi ya vurugu na nguli huyo wa hip-hop. Bi Morgan alisema kuwa wakati wa likizo huko Jamaica, alimwona akimburuta Bi Ventura chini ya ukumbi yadi 50 kwa nywele zake kwa sababu alikuwa "akichukua muda mrefu sana bafuni".
0 Comments