Header Ads Widget

AFRIKA KUSINI KUKATA RUFAA DHIDI YA MCHUNGAJI WA NIGERIA ALIYEFUTIWA MASHTAKA YA UBAKAJI

 

Timothy Omotoso

Bw Omotoso alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2017 alipojaribu kuondoka Afrika Kusini.

Miongoni mwa walalamishi wake ni mwanamke aliyesema alibakwa na mchungaji huyo alipokuwa na umri wa miaka 14.

Katika taarifa, waendesha mashtaka wa Afrika Kusini walikubali "hakuna sababu za kisheria za kumzuia" Bw Omotoso kuondoka nchini kufuatia kuachiliwa kwake.

Hata hivyo, ikiwa rufaa hiyo itaruhusiwa, mamlaka itaomba Bw Omotoso arejeshwe Afrika Kusini, taarifa hiyo iliongeza, ikiangazia "mkataba wa nchi mbili wa Nigeria wa kurejeshwa nchini Afrika Kusini".

Baada ya kuachiliwa huru mwezi Aprili, Bw Omotoso pia alikabiliwa na masuala ya uhamiaji, huku Idara ya Masuala ya Ndani ikidai mapema mwezi huu kwamba alikuwa nchini Afrika Kusini kinyume cha sheria.

Mnamo Jumapili, idara hiyo ilitoa taarifa ikisema kuwa Bw Omotoso ameainishwa kama "mtu asiyefaa", kumaanisha kuwa hataweza kurejea nchini kwa miaka mitano.

Shirika la utangazaji la umma la Afrika Kusini limeripoti kuwa mchungaji huyo aliondoka nchini kwa hiari.

Bw Omotoso anaongoza kanisa la Jesus Dominion International ambalo lina matawi nchini Uingereza, Nigeria, Ufaransa na Israel na pia katika maeneo mengi ya Afrika Kusini, kulingana na tovuti yake.

Kesi ya Bw Omotoso iliweka historia ya Afrika Kusini kuwa kesi ya kwanza ya ubakaji yenye hadhi ya juu kutangazwa moja kwa moja.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI