Header Ads Widget

AFISA ALIYEFANYA MSAKO NYUMBA YA DIDDY ATOA USHAHIDI

 Afisa maalum wa Usalama wa Taifa Gerard Gannon anaendelea kutoa ushahidi wake, aliouanza jana.

Anaiambia mahakama kuhusu dawa za kulevya zilizonaswa nyumbani kwa Combs' Miami.

Orodha hiyo inajumuisha kokeini, ketamine, MDMA, methamphetamine, Xanax, na kemikali zilizopatikana katika eneo lenye uyoga.

Gannon anasema baadhi ya tembe za MDMA za rangi tofauti zilizo na muhuri wa nembo maarufu za chapa, ikiwa ni pamoja na baadhi zenye alama za Tesla na nyingine kwa jina la nembo ya mavazi ya "Supreme".

Ventura, ambaye alichumbiana na Combs kwa zaidi ya muongo mmoja, alitoa ushahidi wake wiki iliyopita.

Ndani ya mahakama hiyo, kuna chumba kilichofurika watu kwa ajili ya kufuatilia kesi.

Skrini kubwa za TV zinaonyesha mashahidi na Combs.

Combs awasili mahakamani huku kesi zikiendelea

Sean "Diddy" Combs aliwasili mahakamani, pembeni yake akiwa na timu yake ya wanasheria wakiongozwa na Marc Agnifilo.

Mwanamuziki huyo wa hip-hop anakabiliwa na mashtaka ya ulaghai, ulanguzi wa ngono na usafirishaji ili kujihusisha na ukahaba - madai ambayo anakanusha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI