Na Matukio Daima Media
Wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Luindo, iliyopo Kata ya Mseke, Wilaya ya Iringa Vijijini kando ya barabara kuu ya Iringa – Mbeya, wameipongeza shule hiyo kwa kuwa na huduma bora ya usafiri kwa wanafunzi wake.
Kwa mujibu wa wazazi hao, mabasi ya shule ya Luindo ni ya kisasa, salama, na yanahudumiwa mara kwa mara, jambo linalowapa amani ya moyo katika kuwapeleka watoto wao shuleni kila siku.
Wakizungumza na Matukio Daima Media kwa nyakati tofauti, wazazi hao, akiwemo Samson Kalinga na Wende Sanga, walisema kuwa mabasi ya shule hiyo yameboresha kwa kiasi kikubwa hali ya usafiri kwa watoto, ukilinganisha na shule nyingi za maeneo ya jirani. Kwa mujibu wa wazazi hao, shule nyingi zimekuwa zikitumia mabasi chakavu na yasiyo salama, ambayo yanahatarisha maisha ya watoto, tofauti kabisa na hali ilivyo katika shule ya Luindo.
Samson Kalinga alieleza kuwa: “Ni jambo la kutia moyo kuona shule ya Luindo ikitoa kipaumbele kwa usafiri wa watoto.
"Mabasi yao ni mapya, yamewekewa viti vya usalama (seat belts), na yanaendeshwa na madereva wenye uzoefu. Kama mzazi, unahisi faraja unapoona mtoto wako anasafiri katika mazingira salama.”
Kwa upande wake, Wende Sanga aliongeza kuwa: “Usafiri mzuri unasaidia watoto kufika shuleni kwa wakati na kuchangamka zaidi darasani. Pia unatupunguzia mzigo wa kila siku wa kuwatafuta pikipiki au magari ya kukodi, ambayo mara nyingi hayana viwango vya usalama.”
Wazazi hao pia waliipongeza shule ya Luindo kwa ufaulu wake mzuri katika mitihani ya taifa, jambo ambalo limeongeza mvuto kwa wazazi wengi zaidi kupeleka watoto wao shuleni hapo. Walisema kuwa kiwango cha ufaulu kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka, kutokana na juhudi za walimu.
KWA MAWASILIANO NA LUINDO IRINGA PIGA SIMU
0763337177
0754 767 205
0 Comments