Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Zaidi ya wanafunzi 40 wa Mtaa wa Lunyanywi waliokuwa wakisoma katika shule za msingi Mjimwema,Nazareth,Sinai na Peruhanda Kata ya Mjimwema Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe wameondokana na adha ya kutembea umbali wa takribani KM 4 Kila siku baada ya shule mpya shikizi Lunyanywi kuanza rasmi kwa madarasa ya Awali na La Kwanza.
Diwani wa kata ya Mjimwema Mhe.Nestory Mahenge ambaye ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ameshuhudia wanafunzi wakianza masomo katika shule hiyo wakitolewa katika shule nyingine ambapo amesema Kata yake imefanikiwa kujenga shule Mpya Tatu tangu aingie mamlakani na zimesaidi kupunguza changamoto za Mlundikano wa wanafunzi darasani.
Ofisa Elimu kata ya Mjimwema Hery Kilasi Amewasisitiza wazazi kuwapeleka watoto shule baada ya kufunguliwa kwa shule hiyo huku akitaka washiriki kikamilifu kuwatimizia mahitaji muhimu watoto wao.
Naye katibu wa Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Andreas Mahali amesema Mbunge anatamani kuona shule hiyo inakamilika na sio kuwa shikizi ili iweze kujitegemea.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe John Malle Amesema Halmashauri itahakikisha inakamilisha madarasa yaliyosalia kwa kuwa Elimu ni kipaumbele muhimu zaidi katika maisha ya mwanadamu.
Wakazi wa Lunyanywi akiwemo Matrida Mgedzi na Hilalia Mwalongo Wanakiri kuwa watoto wao walikuwa wanataabika kutembea umbali mrefu na wakati mwingine wanafika shule wamechoka na kushindwa kusoma vizuri.
Shule hiyo imetumia shilingi milioni 101,701,760 kwa kujenga madarasa matatu yaliyokamilika,vyoo matundu sita,boma la madarasa matatu,Msingi wa madarasa matatu na ofisi mbili za
0 Comments