Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Duru zimearifu kuwa kazi kubwa za Maendeleo zilizofanyika katika kipindi Cha miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani zinatosha kumwezesha kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu huku wanawake wakitakiwa kuwahamasisha waliojiandikisha kwenda kupiga kura.
Katika kongamano la kumpongeza Rais Samia kwa kufikisha miaka minne mamlakani chini ya Jumuiya ya wanawake wa CCM UWT wilaya ya Njombe Mlezi wa CCM mkoa wa Njombe na Mjumbe wa kamati kuu CCM taifa Bi.Halima Mamuya amesema Mwaka huu hakuna kura itasalia uraiani na hivyo zote zinapaswa kwenda kwa Dokta Samia na viongozi wa watakaogombea kupitia Chama hicho.
Baada ya CCM taifa kutangaza kuanza kwa mchakato wa ndani wa uchukuaji fomu kugombea nafasi mbalimbali kura za maoni kuanzia mei mosi Mwaka huu Mamuya amewasisitiza viongozi wanaohusika kwenda kusimamiwa vyema mchakato huo ili ulete tija kuelekea uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa wanawake wa CCM UWT wilaya ya Njombe Beatrice Malekela amesema Zaidi ya wanawake 1450 wamekutana kujadili mafanikio ya miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan Mamlakani kwani amefikisha huduma za kijamii hadi kwenye ngazi ya kitongoji
Malekela amesema Katika kipindi hicho Rais Samia amefanikiwa kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima,Kutoa mikopo kwa wanawake na kusambaza umeme nchi nzima kauli iliyoungwa mkono na Mwenyekiti wa UWT mkoa Dokta Scholastica Kevela.
Akizungumza kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Njombe Mbunge wa Jimbo la Lupembe Edwin Swalle amewataka wanawake kutambua mchango mkubwa wa Rais Samia kwani amefanikiwa kupata tuzo ya Kimataifa kwa kupunguza vifo vya wanawake na watoto kwa Asilimia kubwa.
Naye Mbunge wa viti Maalumu mkoa wa Njombe Neema Mgaya amesema kupungua kwa vifo vya wajawazito kwa Asilimia 80 Kumetokana na jitihada kubwa za Rais Samia kujenga zahanati,Vituo vya Afya na Hospitali kila wilaya kwa ajili ya kupambana na changamoto hiyo.
Aidha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga amesema waliombeza Rais Samia kuwa hatoweza kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ukiwemo ujenzi wa Reli ya kisasa SGR sasa amewaonesha kwa vitendo jambo ambalo wanawake wanaweza bila kuwezeshwa.
Hata hivyo wanawake hao wamemchangia Zaidi ya shilingi Milioni 1.2 Rais Samia kwa ajili ya kwenda kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa Mwaka huu
0 Comments