Header Ads Widget

TETESI KUBWA 5 ZA SOKA JIONI HII: BRUNO FERNANDES MBADALA WA DE BRUYNE PALE CITY?

 


Gwiji wa Mashetani Wekundu, Teddy Sheringham ameeleza kwa nini Bruno Fernandes anaweza kuondoka Manchester United kwenda Mnchester City ikiwa ofa ya uhamisho ya "pauni milioni 100" itawasilishwa.

The Red Devils, baada ya kuona nahodha wa klabu yao akihusishwa na kuhamia Real Madrid majira ya kiangazi, walisisitiza kwamba mchezaji huyo wa Ureno hauzwi.

Sheringham, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo kilichoshinda makombe matatu mwaka 1999, ameiambia casinoapps.com: "Unajua, tulichosikia tu kutoka kwa Manchester United ni kwamba kila mchezaji wa kiwango cha juu ana bei yake, hakuna ambaye hawezi kuuzwa kwa sababu ya fedha, basi labda dili la Bruno kujiunga na Manchester City kama De Bruyne Beck linawezekana.

"Manchester United inahitaji kujijenga upya. Klabu ina hali mbaya. Watahitaji pesa kununua wachezaji.

"Ikiwa City watakuja na pauni milioni 100 kwa ajili Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 30, labda wanaweza kufikiria kumuuza".

United na Bayern zapigana vikumbo kwa Verbruggen


Manchester United wanaripotiwa kuungana na Bayern Munich katika harakati zao za kumnunua mlinda mlango wa Brighton mwenye thamani ya pauni milioni 60 Bart Verbruggen

United tayari wamewasiliana na Brighton kujadili upatikanaji wa Verbruggen. Kipa huyo alijiunga na Brighton kutoka Anderlecht mwaka 2023 kwa takriban Euro milioni 20 (pauni milioni 17), na klabu hiyo inasemekana kutafuta angalau mara mbili ya kiasi hicho ikiwa wanataka kuachana na kipa wao chaguo la kwanza. Kwa mkataba unaoendelea hadi Juni 2028, Brighton hawana shinikizo la kumuuza na wana uwezekano wa kudai ada ya pauni milioni 60. (goal.com)

Ryan Gravenberch anaitamani Madrid


Wakala wa Ryan Gravenberch amefichua kwamba nyota huyo wa Liverpool "angependa kucheza" Real Madrid lakini akaeleza kwa nini uhamisho "hauwezekani".

Katika mahojiano na Marca, wakala wa Gravenberch, Jose Rodriguez alitoa muhtasari wa mawazo ya mchezaji huyo na matarajio ya hali ya juu tangu utoto wake. Alifichua kuwa vilabu vikuu vya Ulaya vimekuwa vikivutiwa na mteja wake tangu alipokuwa kijana, huku Barcelona na Real Madrid wakiwa miongoni mwa wawaniaji wake.

West ham yamtaka Aaron Ramsdale


West Ham wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Southampton Aaron Ramsdale majira ya kiangazi, kwa mujibu wa The Times.

Inadaiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ataruhusiwa kuondoka kwa timu iliyoshuka daraja kwa takriban pauni milioni 20, na anataka kusalia kwenye Ligi ya Premia ili kuhakikisha kwamba anahifadhi nafasi yake England.

Makipa wa sasa wa West Ham ni Lukasz Fabianski, ambaye kandarasi yake inamalizika msimu huu wa joto akiwa na umri wa miaka 40, na chaguo la kwanza Alphonse Areola, 32, ambaye amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI