Header Ads Widget

TAWIRI YAPATA HATAZA YA UGUNDUZI WA DAWA YA KUOTESHA NYWELE,KUZUIA NYWELE KUKATIKA


Na. Andrew Chale Matukio Daima App.

TAASISI ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) imetoa taarifa kwa Umma juu ya kupata Hataza ya ugunduzi wa dawa ya kuotesha nywele, kuzuia nywele kukatika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya Kijamii ya TAWIRI imebainisha kuwa:

"Taarifa yetu ililenga kuujulisha umma kuhusu hataza ya ugunduzi, matumizi ya hataza kwa biashara, utengenezaji wa bidhaa na kuwajengea uwelewa Watanzania ili bidhaa itakapokuwa sokoni hivi karibuni wote tunakuwa na uelewa wa pamoja.

Aidha, Kwa sasa tupo kwenye hatua ya kukamilisha Mkataba wa Makubaliano ya Pamoja (Mutually Agreed Terms) na kampuni inayozalisha dawa na vipodozi hizi ili dawa/bidhaa ziwe sokoni.

Baada ya Mkataba wa Makubaliano ya Pamoja kukamilika, tutautangazia Umma dawa hii itapatikana wapi, mapendekezo ya awali tunatarajia kuwa na mawakala watakaoingiza bidhaa hizi na wao kupata wasambazi au wauzaji wa rejareja katika maeneo mbali mbali nchini.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI