Na Hadija Omary
KATIBU wa siasa na uwenezi wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Lindi Bwana Patrick Magalinja amewataka Wananchi wa Mkoa huo kupuuza Maazimio na msimamo wa chama cha siasa cha Demokrasia na Maendeleo chadema wa hakuna Mabadiliko hakuna Uchaguzi (NO reform no election) na kwamba bila kujali msimamo wa chama hicho Uchaguzi upo pale pale
Magalinja ameyasema hayo Jana April 8 alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii ikiwa ni siku chache baada ya viongozi wakuu wa chama hicho cha Chadema kufanya mkutano wa hadhara Katika viwanja vya shule ya Msingi mpilipili Manispaa ya Lindi na kuwaeleza wananchi juu ya Msimamo wa chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu
msimamo wa "No Reforms, No Election" unalenga kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka huu, mpaka kufanyike marekebisho makubwa ya mifumo na sheria za uchaguzi, kwa kile inachodai sheria na mifumo ya uchaguzi iliyopo sasa inaipendelea zaidi chama tawala.
Mgalinja amesema msimamo wa chama cha mapinduzi CCM Katika jambo Hilo la Uchaguzi upo wazi na kwamba wataenda kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kuzingatia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na katiba hiyo kutoa ukomo wa kuongoza kila baada ya miaka mitano
Aidha Magalinja aliwataka wananchi kuto yumbishwa na maneno ya wanasiasa wachache kwani tume itakayosimamia Uchaguzi huu ndio Ile ile iliyosimamia chaguzi za nyuma ambazo wao walishinda na kupata viti vingi vya wabunge na madiwani
Magalinja Amesema wanasiasa hawana nafasi ya kupinga ama kuruka ruka huku Akieleza kuwa njia pekee wanayotakiwa kufanya ni kutumia majukwaa yao ya sasa kupigana kwa hoja na kisha wananchi watachuja hoja gani ipo hai na ipi yenye udhaifu
Mwisho
0 Comments